• HABARI MPYA

  Friday, July 20, 2018

  LIVERPOOL YAMSAJILI ALISSON KWA DAU LA REKODI YA DUNIA

  MBRAZIL, Alisson Ramses Becker, maarufu kama Alisson amekuwa kipa ghali zaidi duniani kihistoria baada ya kujiunga Liverpool kutoka Roma kwa ada ya uhamisho ya Pauni 65.
  Usajili huo unafanya Liverpool iwe imetumie kiasi cha jumla Pauni Milioni 174.45 baada ya awali ya kuwasajili kiungo wa Guinea, Naby Keita, Mbrazil mwingine, Fabinho na Mswisi, Xherdan Shaqiri.
  Alisson amewasili Merseyside Jumatano na kwenda kufanyiwa vipimo vya afya katika eneo la Melwood, wanakofanyia mazoezi Liverpool.
  Amesaini mkataba wa miaka sita kabla ya kupanda ndege binafsi kurejea Italia kukamilisha mapumziko wake. 
  Alisson amekuwa kipa ghali zaidi duniani kihistoria baada ya kujiunga Liverpool kwa ada ya uhamisho ya Pauni 65 kutoka Roma 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAMSAJILI ALISSON KWA DAU LA REKODI YA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top