• HABARI MPYA

  Tuesday, July 03, 2018

  GOR MAHIA YALAZIMISHA SARE NYINGINE KOMBE LA KAGAME

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya soka ya Gor Mahia ya Kenya ikicheza mchezo wa pili leo kwenye Uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 10:00 jioni, imelazimisha sare nyingine ya mabao 2-2 dhidi ya Lydia Ludic.
  Lydia ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya pili mfungaji akiwa ni Kitenge Alexie lakini Gor Mahia ikafanikiwa kupambana na kusawazisha dakika ya saba kupitia kwa Philemon Otieno.
  Ilipofika dakika ya 51 Lydia ya Burundi iliongeza bao la pili mfungaji akiwa ni Dan Wagaluka na bao hilo likawafanya Gor Mahia wacharuke na kutafuta bao la kusawazisha.

  Gor Mahia ilisawazisha dakika ya 90 baada ya kupata penalti ambayo ilifungwa na Tuisenge Jacpues na kuikoa timu hiyo ya Kenya na kipigo kutoka kwa Lydia.
  Matokeo hayo yameifanya Ports kukaa kileleni mwa Kundi B ikiwa na pointi nne ikifuatiwa na Gor Mahia halafu Rayon ambazo zote zina pointi mbili mbili lakini Lydia yenyewe ipo mkiani ikiwa na pointi moja tu.
  Kesho katika michuano hiyo, Vipers ya Uganda itacheza na Kator FC ya Sudan Kusini, halafu Azam FC itavaana na JKU ya Zanzibar wakati APR itacheza na Dakadaha ya Somalia na Simba itacheza dhidi ya Singida United.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GOR MAHIA YALAZIMISHA SARE NYINGINE KOMBE LA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top