• HABARI MPYA

  Wednesday, July 04, 2018

  ENGLAND KUKUTANA NA SWEDEN KATIKA ROBO FAINALI KALI KOMBE LE DUNIA

  Kipa wa England, Jordan Pickford akichupa kuokoa mkwaju wa penalti wa Carlos Bacca wa Colombia na kuipa timu yake ushindi wa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia usiku wa Jumanne Uwanja wa Otkrytiye Arena mjini Moscow, Urusi na sasa itakutana na Sweden katika Robo Fainali. 
  England ilitangulia kwa bao la Harry Kane dakika ya 57 kwa penalti baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Carlos Sanchez, lakini Yerry Mina akaisawazishia Colombia dakika ta tatu ya muda wa nyongeza baada ya dakika ya 90.
  Penalti za England zilifungwa na Kane, Marcus Rashford na Kieran Trippier huku Jordan Henderson pekee akikosa na za Colombia zilifungwa na Radamel Falcao, Juan Cuadrado na Luis Muriel wakati Mateus Uribe na Bacca walikosa 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ENGLAND KUKUTANA NA SWEDEN KATIKA ROBO FAINALI KALI KOMBE LE DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top