• HABARI MPYA

  Friday, July 13, 2018

  ‘FEI TOTO’ AFUNGUKA BAADA YA KUSAINI YANGA; “SINGIDA WALITOA POSA WAKASHINDWA KUMALIZIA MAHARI”

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Mpya wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema yupo tayari kutumikia adhabu endapo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulingana na kitendo cha kusaini timu mbili ikiwemo Singida United pamoja na Yanga kwa wakati mmoja.
  Fei Toto anayetokea JKU ya Zanzibar,  ameseini mkataba wa miaka mitatu Yanga halikadhalika na Singida ambao usajili wa nyota huyo ni kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online, Fei Toto alikiri kusaini mkataba wa awali miaka mitatu na kuchukuwa Million 20 kutoka kwa uongozi wa Singida, lakini pia baadae aliamua kuzungumza na Yanga na kusaini kutokana na uongozi wa klabu hiyo kufuata taratibu za usajili.

  Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema Singida United walimsainisha mkataba wa awali tu, wakashindwa kumalizana naye


  Alisema Singida walimalizana nao mwezi mmoja kabla ya Ramadhani lakini uongozi huo haukufuata taratibu kwa kuzungumza na uongozi wa timu yake ya JKU, jambo ambalo uongozi wa Yanga kuzungumza na uongozi wa timu yake ya zamani na kumalizana halafu kumpa mkataba huo.
  “Ni kweli nimeingia mkataba Yanga baada ya kuzungumza na viongozi wa JKU, hiyo kwa kuwaeleza ukweli na kutakiwa kulipa fedha hizo nilizo kwa Singida. Baadaye kunieleza wamemalizana nao na nikaamua kudondosha saini,” alisema Fei Toto.
  Wakati huo huo JKU ya wamefungwa na Gor Mahia bao 2-0, wafungaji wakiwa Francis Mustaf na Samuel Onyango ambao wameibuka mshindi wa pili katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ‘FEI TOTO’ AFUNGUKA BAADA YA KUSAINI YANGA; “SINGIDA WALITOA POSA WAKASHINDWA KUMALIZIA MAHARI” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top