• HABARI MPYA

    Monday, July 02, 2018

    DAVIS MOSHA ADHAMINI PAMBANO LA SIMBA NA YANGA ZA MAREKANI LITAKALOFANYIKA JULAI 7 DC

    Na Mahmoud Zubeiry, VIRGINIA
    MAKAMU Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Davis Mosha amejitokeza kudhamini mechi ya soka kati ya wapenzi wa Simba na wapenzi wa Yanga miongoni mwa Watanzania waishio nchini Marekani itakayofanyika Julai 7, mwaka huu mjini Washington DC.
    Mratibu wa mchezo huo utakaokwenda sambamba na tamasha la kila mwaka la DMV Old School Reunion, Lucas Mkabu ‘Dj Luke’ ambalo litaanza Julai 6 likifanyika maeneo tofauti amesema kwamba Mosha amejitokeza kudhamini mchezo huo kwa kutoa vifaa vya michezo.
    “Kwake Mosha hii si mara ya kwanza, amekuwa akidhamini mara kadhaa, na sasa hivi tayari amekwishatuhakikishia kutuletea vifaa vya michezo, yaani jezi za kisasa mpya kabisa zitakazogawiwa kwa timu zote mbili kwa ajili ya mchezo huo,”amesema Dj Luke, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Tanzania waishio maeneo ya Washington DC, Maryland na Virginia uitwao DMV.

    Davis Mosha amedhamini tena mechi ya Simba na Yanga za Marekani itakayofanyika Julai 7 mjini Washington DC

    Luke amesema mechi hiyo itaanza Saa 10:00 jioni kwa saa za Marekani na itafanyika Uwanja wa 830 Ridge Rd, SE Washington, DC 20019 na rekodi inaonyesha wapenzi wa Yanga wamekuwa wakiitambia Yanga.
    Amesema nyota wa Bongo Muvi, Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ ni miongoni mastaa ambao wanatarajiwa kupambana burudani hizo ambazo zitapambwa na starehe, vyakula, vinywaji, Fasheni, Michezo na Nyama choma.
    Ijumaa ya Julai 6 hadi 8 mambo yatakuwa Oxford Center, 9700 Martin L King Jr Hwy, Lanham, MD 20706 kabla ya kumalizia kwa disko la nguvu kuanzia Saa 3:00 usiku DMV International VIBE kwa kiingilio cha dola 50 ambacho kitaambatana na pfa ya kinywaji.
    Jumamosi ya Julai 7 kuaniza Saa 4:00 asubuhi litafanyika Bonanza la Basketball viwanja vya 830 Ridge Rd, SE mjini Washington, DC 20019 kabla ya mchezo wa Simba na Yanga kuchukua nafasi 830 Ridge Rd, SE mjini Washington, DC 20019.
    Na kuanzia Saa 3:00 usiku litaporomoshwa disko la nguvu la “Old School Reunion Party” ambalo halijawabui kutokea chini ya ma DJ wakali Amerika Kaskazini, Dj Luke Joe na Dj Dennis The Funkhouse na siku mambo yote gharama yake itakuwa dola 80 pamoja na chakula na vinywaji kutwa kucha.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DAVIS MOSHA ADHAMINI PAMBANO LA SIMBA NA YANGA ZA MAREKANI LITAKALOFANYIKA JULAI 7 DC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top