• HABARI MPYA

  Wednesday, July 04, 2018

  CAF YAIIDHINISHA MTIBWA SUGAR KUCHEZA KOMBE LA SHIRIKISHO MWAKANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetuma barua ya ufafanuzi kuhusu adhabu ya Mtibwa Sugar.
  Katika barua ya CAF kwenda kwa Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred, imesema Mtibwa Sugar wanaruhusiwa kushiriki katika mashindano ya Kombe la Shirikisho lakini ikiwataka kuwasilisha nyaraka zinazothibitisha kulipwa kwa faini ya dola za Kimarekani 1500 pamoja na fidia kwa timu ya Santos ya Afrika Kusini.

  Mtibwa Sugar ilifungiwa kushiriki mashindano ya kimataifa April 2004 wakifungiwa miaka 3 na faini ya dola 1500.
  TFF inafanya juhudi kubwa kuhakikisha jambo hilo linamalizika kabla ya Julai 20,2018 tarehe ya mwisho iliyotolewa na CAF nyaraka hizo kuwa zimewasilishwa.
  Mtibwa Sugar ndio mabingwa wa Azam Sports Federation Cup na wataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Africa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YAIIDHINISHA MTIBWA SUGAR KUCHEZA KOMBE LA SHIRIKISHO MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top