• HABARI MPYA

  Wednesday, July 04, 2018

  SIMBA SC, TFF WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA PROFESA MAJI MAREFU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mmoja wa Wanachama wake mwandamizi,  Stephen Ngonyani kilichotokea usiku wa kuamkia jana Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
  Mh Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu atakumbukwa sana na Wanasimba kwa mchango wake mkubwa katika masuala mbalimbali yaliyoiwezesha klabu yetu kufika hapa ilipo.
  Hivyo kaimu Rais wa klabu, Salum Abdallah Muhene, viongozi wote, wanachama, wachezaji na mashabiki wote wanatoa pole kwa Spika wa Bunge na Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuondokewa na Mbunge mwenzao ambae alikuwa akiwakilisha wananchi wa Jimbo la Korogwe vijijini.
  Simba pia wametoa pole kwa Wananchi wote wa jimbo la Korogwe, Ngonyani alilitumilkia kwa uadilifu mkubwa.
  Sambamba na hayo klabu inawapa pole sana familia na wafiwa wote na inawaomba wawe na subira kwenye kipindi hiki kigumu kwao.
  Wakati huo huo: Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Ndugu Wallace Karia amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini,Stephen Ngonyani “Profesa Majimarefu” aliyefariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili usiku wa kuamkia jana.
  Rais wa TFF Ndugu Karia amesema Profesa Majimarefu alikuwa mwanamichezo kwa vitendo akishiriki katika mambo mbalimbali ya Mpira wa Miguu.
  “Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Profesa Majimarefu ambaye hakika alikuwa mwanamichezo wa kweli akishiriki kwa vitendo hata katika jimbo lake la Korogwe Vijijini,Kwa niaba ya TFF natoa pole kwa Familia,ndugu,Jamaa na marafiki” alisema Rais wa TFF Ndugu Karia.
  Aidha Rais wa TFF Ndugu Karia amepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa Polisi Dar Awadh Kilewa na kwa niaba ya TFF ametoa pole kwa wafiwa,familia,ndugu,timu ya Polisi Dar na marafiki.
  Amesema kifo cha Awadh kimeshtua hasa kutokana na kuwa bado mchango wake ulihitajika katika Mpira wa Miguu.
  “Mchango wa Awadh kwenye Mpira wa Miguu bado ulikuwa ukihitajika katika Timu yake ya Polisi na mpira wa miguu kiujumla,Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, Amina.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC, TFF WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA PROFESA MAJI MAREFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top