• HABARI MPYA

    Wednesday, April 23, 2014

    SAMATTA NA ULIMWENGU WAJITOA TAIFA STARS

    Na Baby Akwitende, Dar es Salaam
    WACHEZAJI wawili wa kimataifa, Mbwana Samatta, na Thomas Ulimwengu, wanaoichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hawatakuja nchini kuivaa Burundi katika mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji Taifa Stars itakayofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu kutoka Lubumbashi- DRC, Samatta, alisema kuwa wana taarifa ya mchezo huo lakini hawajui kama watakuja kucheza mechi hiyo ambayo haiko kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
    Watatusamehe; Mbwana Samatta kushoto na Thomas Ulimwengu hawatakuja kuichezea Stars Jumamosi dhidi ya Burundi

    Samatta alisema kuwa timu yao inakabiliwa na mechi ya ligi itakayochezwa Jumapili dhidi ya klabu ya Don Bosco hivyo uongozi haujawaeleza lolote kuhusiana na ruhusa ya kurejea nchini kuivaa Burundi.
    "Hatujui kama tutakuja ila taarifa ya hiyo mechi tunayo, huku tuna mechi kesho (leo) na nyingine Jumapili tunaivaa Don Bosco," alisema Samatta ambaye alitua TP Mazembe akitokea Simba.
    Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, ameiambia blog hii leo kwamba wachezaji hao hawatakuja nchini licha ya kuitwa na benchi la ufundi la timu hiyo.
    Wambura alisema kwamba wamewaita kutokana na heshima yao lakini wanafahamu ni vigumu kuwapata siku hiyo.
    "Tumewatangaza katika kikosi lakini hawatakuja," alisema kwa kifupi Wambura. Kikosi kamili kilichoitwa kujiandaa na mechi hiyo na tayari wako kambini ni pamoja na makipa, Aishi Manula na Mwadini Ally wa Azam FC na Deogratias Munishi wa Yanga, wakati mabeki ni Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kevin Yondani (Yanga SC) na Said Mourad (Azam).
    Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba) wakati washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samatta (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
    Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).
    Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA NA ULIMWENGU WAJITOA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top