• HABARI MPYA

    Friday, April 18, 2014

    BARCELONA SASA RADHI KUMUUZA MESSI

    MSHAMBULIAJI Lionel Messi anaamini Barcelona sasa inamchukulia kama mtu wa kuuzwa na si tena nyota asiyegusika katika kikosi chao, imeripotiwa chaneli ya Televisheni ya Esport3 ya Katalunya.
    Kusuasua kwa mazungumzo ya kuongeza mkatab baina ya mchezaji huyo na klabu ni kielelezo cha kwa nini Messi anafikiria muda wake umekwisha Barcelona.
    Inaelezwa kwamba Wajumbe wa bodi wanaamini mchezaji huyo ana thamani zaidi ya kuuzwa kwa sasa kuliko kuendelea kuwatumikia uwanjani, jambo ambalo Messi analitambua pia na anaamini ni juu ya Barcelona kuhusu Mkataba wake unaomalizika mwaka 2018.

    Mwisho? Lionel Messi anaweza kuondoka Barcelona kutokana na kusuasua kwa mazungumzo ya Mkataba mpya

    Paris Saint-Germain inaweza kuwa tayari kumlipa mchezaji huyo mshahara wa Pauni Milioni 205, na kutokana na mpango wa ujenzi wa Uwanja mpya unaoweza kuigharimu Barcelona Pauni Milioni 493, inawezekana klabu hiyo ikafanya uamuzi usiofikirika na kumuuza mchezaji huyo ambaye amekuwa Barcelona tangu ana umri wa miaka 13.

    Messi anataka kubaki Barcelona hadi atakapofikiri wakati wa kurejea klabu yake ya kwanza, Newell’s Old Boys ya Argentina umewadia, lakini Barcelona inaweza kumuuza kwa klabu nyingine ya Ulaya kati ya PSG hata Manchester City.
    Top of the world: Messi with the Ballon d'Or trophy in 2012
    Babu kubwa duniani: Messi akiwa na tuzo ya Ballon d'Or ya mwaka 2012

    MAFANIKIO YA LIONEL MESSI BARCELONA

    2004:Mechi 420 mabao 351
    La Liga 2004-5, 2005-6, 2008-9, 2009-10, 2010-11, 2012-13
    Kombe la Mfalme: 2009, 2012
    Ligi ya Mabingwa 2006, 2009, 2011
    Rais wa sasa wa Barcelona, Josep Bartomeu alitaka kumpa mkataba mpya Messi kabla ya Fainali za Kombe la Dunia, lakini mchezaji huyo inafahamika anataka malipo ya Pauni Milioni 20.5 kwa mwaka na klabu inataka nusu ya haki ya matumizi ya picha zake, wakati kwa sasa mchezaji huyo anamiliki haki zote.
    Kushindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na fainali ya Kombe la Mfalme kwa mara ya kwanza vimeifanya bodi ifikirie uamuzi wa kumpiga bei.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCELONA SASA RADHI KUMUUZA MESSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top