• HABARI MPYA

    Thursday, November 07, 2013

    YANGA YAUA 3-0 NA KUPAA KILELENI LIGI KUU BARA, AZAM 3-3 NA MBEYA CITY CHAMAZI

    Mpira nyavuni; Bao la kwanza la Azam leo Chamazi
    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    YANGA SC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Azam FC ikitoka sare ya 3-3 na Mbeya City, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 
    Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabao ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva dakika 23, Mrisho Ngassa dakika ya 23 na Jerry Tegete dakika ya 53.
    Yanga; Deogratius Munishi, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Simon Msuva, Frank Domayo/Lusajo Reliants, Mrisho Ngasa, Hamis Kiiza/Hamisi Kiiza, Haruna Niyonzima/Said Bahanunzi dk79.
    Oljoro JKT; Damas Malipesa, Majaliwa Mbaga, Yusuph Machogote, Shaibu Nayopa, Nurdin Seleman, Expedito Kiduko, Swalehe Idd, Issa Kandulu, Babu Ally na Sanu Mwaseba.
    Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Azam wakitangulia kupata bao kupitia kwa Humphrey Mieno dakika ya 13 na Mbeya City wakasawazisha kupitia kwa Mwagane Yeya ‘Morgan’ dakika ya 30.
    Ngassa ameifungia Yanga Taifa leo

    Mabao yote yalitokana na mipira ya pembeni, Mieno akifunga kwa kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Farid Mussa nje kidogo ya 18, kufuatia kipa David Burhan kudakia nje ya eneo lake na Mwagane aiunganisha krosi ya Deus Kaseke.
    Kipindi cha pili, Mbeya City walitangulia kupata bao dakika ya 52 Mwagane Yeya tena akiunganisha kwa kichwa krosi ya Steven Mazanda, lakini John Bocco ‘Adebayor’ akaisawazishia Azam dakika ya 60 akiunganisha krosi ya Kipre Tchetche.
    Mwagane tena akaifungia Mbeya City kwa shuti kali dakika ya 73 baada ya pasi ya Mazanda, lakini Khamis Mcha ‘Vialli’ aliyetokea benchi aliisawazishia Azam dakika ya 83, dakika tatu tu tangu aingie kuchukua nafasi ya Farid Mussa. 
    Kwa matokeo hayo, Yanga inamaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 28 na kupaa kileleni, wakati Azam inashuka nafasi ya pili kwa pointi zake 27 sawa na Mbeya City, lakini inabebwa kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
    Azam; Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Salum Abubakar, Kipre Tchetche, John Bocco/Joseph Kimwaga 72, Humphrey Mieno na Farid Mussa/Khamis Mcha dk80. 
    Mbeya City; David Burhan, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius, Yussuf Abdallah, Anthony Matogolo, Mwagane Yeya, Steven Mazanda/Alex Sethi dk90, Paul Nonga/Francis Castor, Deus Kaseke na Richard Peter/Peter Mapunda dk46.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YAUA 3-0 NA KUPAA KILELENI LIGI KUU BARA, AZAM 3-3 NA MBEYA CITY CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top