• HABARI MPYA

    Tuesday, February 03, 2009

    HUU NI WASIA WANGU KWENU AKINA TIBAIGANA

    MWISHONI mwa wiki, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitaja viongozi walioteuliwa kwenye Kamati ndogo za shirikisho hilo. Kamanda mstaafu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum, Dar es Salaam, Alfred Tibaigana akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu akichukua nafasi ya Said El Maamry.
    Makamu mwenyekiti ni Mustapha Kambona na wajumbe wa kamati hiyo ni Mussa Azzan ‘Zungu’, ambaye ni Mbunge wa Ilala, Yussuf Nzowa, Jamal Bayser, Llyod Nchunga na Mohamed Msomali.
    Aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF, Crescentius Magori atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Habari na Masoko akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti, William Kalaghe na Wajumbe Amin Bakhresa, Boniface Wambura, Angetile Osiah, Mohammed Nassor na Philemon Ntahilaja.
    Kamati ya Sheria, Maadili na Wachezaji itakuwa chini ya Mwenyekiti Alex Mgongolwa, atakayesaidiwa na Makamu wake Hussein Mwamba, Wajumbe ni Iman Madega, Venance Mwamoto, Omary Gumbo na Ismail Aden Rage.
    Aidha, Makamu wa Kwanza wa rais wa TFF, Athumani Nyamlani atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango, wakati Makamu wake atakuwa Amir Rosham na Wajumbe Samuel Nyalla, Eliud Mvella, Andrew Simkoko, Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan na Yakub Kidula.
    Kamati ya Mashindano itaongozwa na Makamu wa Pili wa Rais TFF, Ramadhan Nassib, akisaidiwa na Makamu wake, Wallace Kiriab wakati Wajumbe watakuwa Lawrance Mwalusako, Said George, Ahmed Yahya, Leopold Tasso na Salum Chambuso.
    Kamati ya Ufundi na Maendeleo itakuwa chini ya Mwenyekiti Teofrid Sikazwe, Makamu Mwenyekiti, Khalid Mohammed, wakati Joseph Mapunda, Charles Boniface, Elizabeth Kalinga, Charles Masanja na Arthur Mwambeta ni Wajumbe.
    Kamati ya Vijana itakuwa chini ya Mwenyekiti Ahmed Mgoyi, Makamu wake, Athumani Kambi na Wajumbe Ally Mtumwa, Daudi Yassin, John Mwangakala, Aaron Sokoni na Charles Mbuge.
    Kamati ya Rufani itakuwa chini ya Mwenyekiti, Profesa Mgongo Fimbo, Makamu wake, Ong’wanuhama Kibuta na Wajumbe Iddi Kipingu, Mohammed Misanga (Mbunge), Mshindo Msolla, Henry Tandau na Jamal Rwambow.
    Kamati ya Uchaguzi itakuwa chini ya Mwenyekiti, Deo Lyato, Makamu wake, Hamidu Mbwezeleni na Wajumbe Moses Kaluwa, Hassan Dyamwalle na Kitwana Manara, wakati Kamati ya Ukaguzi wa Ndani itakuwa chini ya Mwenyekiti Khalifa Mgonja na Makamu wake, Muhsin Balhabou.
    DIMBA tunapenda kuchukua fursa hii kuipongeza TFF chini ya rais wake, Leodegar Tenga kwa uteuzi wa Kamati hizi, ambazo kimsingi zitawasaidia katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya soka nchini.
    Lakini pamoja na hilo, DIMBA tunachukua fursa hii kutoa nasaha kwa walioteuliwa kwenye Kamati mbalimbali, wajue fika jukumu lao ni kuisaidia TFF na si kwenda kuwa wapinzani wa shirikisho hilo na kujikuta wanakuwa kikwazo cha utekelezaji wa sera za maendeleo.
    Hiki ni kipindi cha kusimamia mabadiliko katika soka nchini, kwa gharama zozote zile lazima kanuni zilizowekwa kusimamia mchezo huo ziheshimiwe na mtu yeyote asipewe mwanya wa kuvuruga dhamira hiyo.
    Aidha, walioteuliwa kwenye Kamati hizi wanapaswa kujitambua kwamba wamepewa dhamana kwa ajili ya soka Tanzania, wasije kujisahau na kujikuta wanakuwa manazi ndani ya TFF na kugeuka kuwa mabalozi wa klabu wazipendazo. Tunasema hivi kwa sababu tumekwishaona kipindi kilichopita, watu wanatumia vibaya madaraka yao.
    DIMBA tunataka walioteuliwa kwenye Kamati hizi wafanye kazi kwa maadili na kusaidia dhamira ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya soka Tanzania.
    Pamoja za kuzitakia heri Kamati hizi na TFF kwa ujumla, pia tunaahidi kuendelea kuwa bega kwa bega na TFF katika jitihada za kukuza mchezo huu nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HUU NI WASIA WANGU KWENU AKINA TIBAIGANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top