• HABARI MPYA

    Tuesday, April 20, 2021

    YANGA SC WAITANDIKA GWAMBINA FC 3-1 NA KUJIIMARISHA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA

     

    TIMU ya Yanga SC leo imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Gwambina FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Ditram Nchimbi dakika ya 19, Bakari Mwamnyeto dakika 52 na Saido Ntibanzokiza dakika ya 90 na ushei, wakati la Gwambina limefungwa na Jimson Mwanuke dakika ya 49.
    Kwa ushindi huo, Yanga SC imefikisha pointi 57 baada ya kucheza mechi 26 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi nne mkononi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAITANDIKA GWAMBINA FC 3-1 NA KUJIIMARISHA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top