• HABARI MPYA

    Thursday, April 15, 2021

    MAN CITY YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA

     

    TIMU ya Manchester City ya England imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Borussia Dortmund usiku wa jana Uwanja wa Signal-Iduna-Park Jijini Dortmund, Ujerumani.
    Jude Bellingham alianza kuifungia Borussia Dortmund dakika ya 15, kabla ya Man City kutoka nyuma kwa mabao ya Riyad Mahrez dakika ya 55 kwa penalti na Philip Foden dakika ya 75.
    Manchester City wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-2 baada ya kushinda 2-1 pia kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Etihad na watakutana na PSG ya Ufaransa iliyowatoa waliokuwa mabingwa watetezi, Bayern Munich.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top