• HABARI MPYA

  Friday, July 06, 2018

  SHAABAN IDDI AMFUATA FARID MUSSA TENERIFE, ASAINI MIAKA MIWILI KWA MKOPO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa Azam FC, Shaaban Iddi Chilunda amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na CD Tenerife ya Daraja la Kwanza nchini Hispania.
  Meneja wa Azam FC, Philipo Alando ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba klabu hiyo ya Santa Cruz mjini Tenerife, visiwa vya Canary imeamua kumchukua mchezaji huyo, baada ya kuvutiwa na mchezaji mwingine wa Tanzania, Farid Mussa.
  Alando amesema kwamba ni wiki mbili tu tangu Tenerife imnunue moja kwa moja mchezaji mwingine wa zamani wa Azam FC, winga Farid Mussa ambaye pia walimchukua kwanza kwa mkopo miaka miwili iliyopita.
  Shaaban Iddi amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na CD Tenerife ya Daraja la Kwanza nchini Hispania
   

  Alando amesema kwamba uongozi wa Azam FC imetoa baraka zake zote kwa mchezaji huyo kwenda kujaribu maisha mapya Ulaya baada ya kazi nzuri katika misimu yake miwili ya kuwa kikosi cha kwanza cha Azam FC.
  Shaaban Iddi ambaye atatimiza miaka 20 Julai 20 mwaka huu tangu azaliwe mwaka 1998, alijiunga na akademi ya Azam FC Jumamosi ya Julak 21, mwaka 2012 kabla ya miaka miwili baadaye kupandishwa kikosi cha kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHAABAN IDDI AMFUATA FARID MUSSA TENERIFE, ASAINI MIAKA MIWILI KWA MKOPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top