• HABARI MPYA

  Saturday, July 07, 2018

  PSG YAMTAMBULISHA BUFFON KIPA WAO MPYA MSIMU UJAO

  Gianluigi Buffon amejiunga na Paris Saint-Germain  kama mchezaji huru akitokea Juventus 

  WASIFU WA BUFFON 

  Mwaka
  1995-2001
  2001-2018
  2018— 
  Klabu
  Parma
  Juventus
  PSG 
  Mechi
  168
  509
   

  Mataji

  Serie A: 2001–02, 2002–03, 2011–12, 2012–13, 2013–14, 2014–15, 2015–16, 2016–17, 2017–18.
  Coppa Italia: 1998-99, 2014–15, 2015–16, 2016–17, 2017–18
  UEFA Cup: 1998–99 
  World Cup: 2006
  KLABU ya Paris Saint-Germain imethibitisha kumsajili kipa mkongwe, Gianluigi Buffon kama mchezaji huru akitokea Juventus.
  Klabu hiyo ya Ufaransa imetoa video ya utambulisho wa Buffon akiwa amevalia jezi mpya ya kipa ya msimu wa 2018-2019 ya klabu hiyo.
  Buffon amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo bingwa ya Ligue 1 wenye kipengele cha kuongezewa miezi mingine 12 kama ataamua kuendelea na kazi Parc des Princes kwa mara ya pili. 
  Kipengele hicho kikitimia itamfanya acheze hadi atakapofikisha umei wa miaka 42. Mtaliano huyo ameiambia tovuti ya klabu kwamba: "Kwa hisia kubwa za furaha najiunga na na Paris Saint-Germain.
  Kwa mara ya kwanza katika historia yangu, ninaiacha  nchi yangu na ni mpango huu unaonifanya nichukue maamuzi haya,". 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PSG YAMTAMBULISHA BUFFON KIPA WAO MPYA MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top