• HABARI MPYA

  Thursday, July 05, 2018

  GOR MAHIA YAZINDUKA KOMBE LA KAGAME YAIFUNGA PORTS 2-0

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MECHI za mwisho za hatua ya makundi za Kombe la Kagame zimechezwa usiku huu kwenye viwanja viwili vya Taifa na Azam Complex uliopo Chamazi Dar es Salaam.
  Ikicheza mechi yake ya Kundi B kwenye Uwanja wa Taifa, Gor Mahia ya Kenya imeifunga AS Ports ya Djibouti mabao 2-0 na kumaliza jinamizi la sare lililokuwa likiwaandama.
  Gor Mahia sasa imefikisha pointi tano katika Kundi B huku Ports ikiwa na pointi nne. Mabao ya Gor Mahia katika mchezo huo yamefungwa na Otieno Philemon dakika ya 13 akipokea pasi ya Wafula Innocent na bao la pili lilifungwa na Momanyi Charles dakika ya 40 akiunga kona ya Godfrey Walusimbi.

  Katika mchezo mwingine uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Rayon Sports ya Rwanda imeifunga Lydia Ludic ya Burundi mabao 3-1.
  Lydia ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 20 mfungaji akiwa ni Dan Wagaluka kwa njia ya penalti lakini mabao ya Rayon yamefungwa na Rwatubyaye Abdul dakika ya 29, Muhire Kelvin dakika ya 49 na Pierre Kwizera aliyefunga dakika ya 72.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GOR MAHIA YAZINDUKA KOMBE LA KAGAME YAIFUNGA PORTS 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top