• HABARI MPYA

  Monday, December 19, 2016

  YANGA YAPANGWA NA AZAM, SIMBA NA URA KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imepangwa Kundi B katika michuano ya kila mwaka ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar pamoja na Azam FC ya Dar es Salaam, Jamhuri na Zimamoto zote za Zanzibar.
  Katika michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuanzia Desemba 30 hadi Januari 13 mwakani, Kundi A lina timu za Simba ya Dar es Salaam, Taifa ya Jang’ombe, Jang’ombe Boys, KVZ na mabingwa watetezi, URA ya Uganda.
  Michuano hiyo itaanza Desemba 30 mwaka huu kwa Taifa ya Jang'ombe kumenyana na Jang'ombe Boys kuanzia Saa 2:30 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Kitimutimu kitaanza rasmi Januari 1 kwa mchezo kati ya mabingwa watetezi, URA dhidi ya KVZ kuanzia Saa 10:00 jioni kabla ya Simba kumenyana na Taifa ya Jang'ombe Saa 2:30 usiku.
  Mechi za Kundi B zitaanza Januari 2, mwakani (2017) kwa Azam FC kumenyana na Zimamoto kuanzia Saa 10:00 jioni kabla ya Yanga kumenyana na Jamhuri Saa 2:30 usiku.

  RATIBA KAMILI KOMBE LA MAPINDUZI.
  Desemba 30, 2016
  Taifa Jang'ombe vs Jang'ombe Boys (Saa 2:30 usiku)
  Januari 1, 2017
  KVZ VS URA (Saa 10:00 jioni)
  Simba vs Taifa Jang'ombe (Saa 2:30 usiku)
  Januari 2, 2017 
  Azam vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni 
  Yanga vs Jamhuri (Saa 2:30 usiku)
  Januari 3, 2017 
  Jang'ombe Boys vs URA (Saa 10:00 jioni) KVZ vs Simba (Saa 2:30 usiku)
  Januari 4, 2017 
  Zimamoto vs Yanga (Saa 10:00 jioni)
  Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.
  Januari 5, 2017
  KVZ vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)
  Simba vs URA (Saa 2:30 usiku)
  Januari 6, 2017
  Taifa Jang'ombe vs KVZ (Saa 2:30 usiku)
  Januari 7, 2017
  Jamhuri vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni)
  Yanga vs Azam (Saa 2:30 usiku)
  Januari 8, 2017 
  Simba vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni) Taifa Jang'ombe vs URA (Saa 2:30 usiku).
  Januari 10, 2017
  Nusu Fainali ya kwanza (Saa 10: 00 jioni)
  Nusu Fainali ya Pili (Saa 2:30 usiku)
  Januari 13, 2017
  FAINALI
  Saa 2: 30 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAPANGWA NA AZAM, SIMBA NA URA KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top