• HABARI MPYA

    Monday, December 19, 2016

    TEVEZ GHAFLA KUWAFUNIKA RONALDO NA MESSI KWA MALIPO

    MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Carlos Tevez anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa fedha nyingi kwenda China licha ya mashabiki wa Boca Juniors kumuomba kwa hisia kali jana usiku shujaa wao abaki.

    Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 32 na mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Argentina anatarajiwa kusaini mkataba na klabu ya Ligi Kuu ya China, Shanghai Shenhua kwa mshahara wa Pauni 615,000 kwa wiki.

    Na mchezaji huyo wa zamani wa West Ham, Manchester United na Manchester City alitumia fursa hiyo kuwaaga mashabiki wa klabu yake ya kwanza kuchezea wakiifunga Colon mabao 4-1 huko La Bombonera.

    Akiwa amefunga bao la pili siku hiyo, Tevez alitolewa dakika ya 90 kupewa fursa ya kuwaaga mashabiki majukwaani.

    Shabiki mmoja alimkimbilia Tevez uwanjani na kumpigia magoti akimsihi asiondoke, kabla ya kuondolewa na walinzi.

    Majukwaani mashabiki walionyesha upendo mkubwa kwa Tevez wakiwa wamebeba mabango yenye kusomeka; 'usiondoke Carlos!'


    Tevez atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani Pauni 615,000 kwa wiki ni sawa Pauni Milioni 31.98 kwa mwaka na aatafutaiwa na Mbrazil Oscar wa Shanghai SIPG anayelipwa  Pauni 400,000 kwa wiki, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid Pauni 365,000 kwa wiki, Lionel Messi wa Barcelona Pauni 365,000 kwa wiki na Gareth Bale wa Real Madrid Pauni 346,000 kwa wiki.
    Shabiki akiwa amempigia magoti Tevez kumsihi asiondoke Boca Juniors  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    WACHEZAJI 10 WANAOLIPWA ZAIDI DUNIANI 

    1) Carlos Tevez (Shanghai Shenhua) Pauni 615,000 kwa wiki sawa na Pauni Milioni 31.98 kwa mwaka
    2) Oscar (Shanghai SIPG) Pauni 400,000 kwa wiki sawa na Pauni Milioni 20.8 kwa mwaka
    3=) Cristiano Ronaldo (Real Madrid) Pauni 365,000 kwa wiki sawa na Pauni Milioni 19 kwa mwaka
    3=) Lionel Messi (Barcelona) Pauni 365,000 kwa wiki sawa na Pauni Milioni 19 kwa mwaka
    5) Gareth Bale (Real Madrid) Pauni 346,000 kwa wiki sawa na Pauni Milioni 18 kwa mwaka
    6) Hulk (Shanghai SIPG) Pauni 317,000 kwa wiki sawa na Pauni Milioni 16.5 kwa mwaka
    7) Paul Pogba (Manchester United) Pauni 290,000 kwa wiki sawa na Pauni Milioni 15 kwa mwaka
    8) Neymar (Barcelona) Pauni 289,000 kwa wiki sawa na Pauni Milioni 15 kwa mwaka
    9=) Graziano Pelle (Shandong Luneng) Pauni 260,000 kwa wiki sawa na Pauni Milioni 13.5 kwa mwaka
    9=) Wayne Rooney (Manchester United) Pauni 260,000 kwa wiki sawa na Pauni Milioni 13.5 kwa mwaka.
    *Uhamisho unatarajiwa kukamilishwa Januari*
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TEVEZ GHAFLA KUWAFUNIKA RONALDO NA MESSI KWA MALIPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top