• HABARI MPYA

  Monday, December 12, 2016

  SIMBA NA MTIBWA KIINGILIO BUKU TANO CHAMAZI

  Na Mwandishi Wegu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC itacheza na Mtibwa Sugar leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo maalum wa kirafiki wa kujaribu wachezaji wapya.
  Mchezo huo utakaoanza Saa 10:00 jioni ni maalum kwa kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog kuwajaribu kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei wote kutoka Ghana. 
  Agyei aliyekuwa anachezea Medeama SC ya kwao amekwishasajiliwa, wakati Kotei aliyekuwa anacheza Oman bado anajaribiwa na huenda mchezo wa leo ukaamua hatima yake.
  Timu zote mbili zinajiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba wakifungua dimba na Ndanda FC mjini Mtwara Desemba 18 na Mtibwa Sugar wakianza na Ruvu Shooting.
  Ikumbukwe Simba SC ilimalizia kileleni mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwa pointi zake 35, mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga wakati Mtibwa ilimalizia nafasi ya tano kwa pointi zake 23 nyuma ya Azam pointi 25 na Kagera Sugar 24.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA MTIBWA KIINGILIO BUKU TANO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top