• HABARI MPYA

  Monday, December 12, 2016

  ARSENAL NA BAYERN MUNICH 16 BORA LIGI YA MABINGWA

  Arsene Wenger ataiongoza timu yake dhidi ya Bayern Munich tena katika Ligi ya Mabingwa Ulaya PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  REKODI YA KARIBUNI YA ARSENAL NA BAYERN

  2012-13 (16 Bora)
  Arsenal 1-3 Bayern Munich
  Bayern Munich 0-2 Arsenal
  2013-14 (16 Bora)
  Arsenal 0-2 Bayern Munich
  Bayern Munich 1-1 Arsenal
  2015-16 (makundi) 
  Arsenal 2-0 Bayern Munich
  Bayern Munich 5-1 Arsenal  
  TIMU ya Arsenal itamenyana na Bayern Munich katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  The Gunners waliongoza kundi lao kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2011/2012 wakiipiku Paris Saint-Germain, lakini malipo yake ni kukutana na vigogo wa Ulaya.
  Bayern Munich ilimaliza nafasi ya pili nyuma ya Atletico Madrid katika kundi lake.
  Kocha Pep Guardiola wa Manchester City, aliyemaliza nafasi ya pili nyuma ya Barcelona, amepata timu nafuu kudogo, Monaco ya Ufaransa. Leicester, wakicheza kwa mara ya kwanza Ligi ya Mabingwa, wamepangwa na Sevilla. 

  RATIBA YA LIGI YA MABINGWA 16 BORA... 

  Manchester City vs Monaco 
  Mechi ya kwanza: Februari 21 - Manchester
  Marudiano: Machi 15 - Monaco
  Real Madrid vs Napoli
  Mechi ya kwanza: Februari 15- Madrid
  Marudiano: Machi 7 - Naples
  Benfica vs Borussia Dortmund
  Mechi ya kwanza: Februari 14 - Lisbon
  Marudiano: Machi 8 - Dortmund
  Bayern Munich vs Arsenal 
  Mechi ya kwanza: Februari 15 - Munich
  Marudiano: Machi 7 - London
  Porto vs Juventus
  Mechi ya kwanza: Februari 22 - Porto
  Marudiano: Machi 14 - Turin
  Bayer Leverkusen vs Atletico Madrid
  Mechi ya kwanza: Februari 21 - Leverkusen 
  Marudiano: Machi 15 - Madrid 
  Paris Saint Germain vs Barcelona
  Mechi ya kwanza: February 14 - Paris
  Marudiano: Machi 8 - Barcelona 
  Sevilla vs Leicester City 
  Mechi ya kwanza: Februari 22 - Seville
  Marudiano: Machi 14 - Leicester 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL NA BAYERN MUNICH 16 BORA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top