• HABARI MPYA

    Thursday, January 29, 2015

    TFF YAHADHARISHA MGOGORO WA ZFA KORTINI

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF)l imepokea kwa masikitiko taarifa za kuwepo tena kortini kwa kesi dhidi ya uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), jambo ambalo linaweza kuathiri ushiriki wa timu za Zanzibar kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, na Kombe la Shirikisho.
    Mwishoni mwa mwaka jana, TFF ilihadharisha juu ya masuala ya mpira wa miguu kupelekwa mahakamani, kwani kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za uendeshaji mpira wa miguu ambazo zinakataza masuala ya mchezo huo kupelekwa katika mahakama za kawaida.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi katikati

    Kutokana na hali hiyo, TFF iliiandikia barua ZFA kutaka mgogoro huo uondolewe kortini na yenyewe kuridhia kuwa tayari kupeleka ujumbe Zanzibar ili ukutane na pande zinazohusika.
    Pia TFF ilisema timu za Tanzania Bara zisingeruhusiwa kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 iwapo kesi hiyo ingeendelea kuwepo kortini na kutaka iondolewe bila masharti yoyote.
    ZFA iliithibitishia TFF kuwa kesi hiyo imeondolewa kortini bila masharti, hivyo timu za Tanzania Bara kuruhusiwa kushiriki katika michuano ya Kombe la Mapinduzi. Ni muhimu suala hilo likashughulikiwa haraka ili kutohatarisha ushiriki wa timu za KMKM na Polisi kwenye michuano hiyo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAHADHARISHA MGOGORO WA ZFA KORTINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top