• HABARI MPYA

    Wednesday, January 28, 2015

    RONALDO AFUNGIWA MECHI MBILI KWA 'UBONDIA' LA LIGA

    MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amefungiwa mechi mbili baada ya kumpiga ngumi beki Jose Angel Crespo Cordoba Jumamosi, Real Madrid ikishinda 2-1 kwa mbinde katika La Liga.
    Kwa adhabu hiyo, Real Madrid itamkosa Ronaldo katika mechi dhidi ya timu ya David Moyes, Real Sociedad Jumamosi na ya nyumbani dhidi ya Sevilla siku tatu baadaye. Atarejea katika mchezo wa ugenini dhidi ya Atletico Madrid wikiendi inayofuata.
    FA ya Hispania imesakamwa ikitakiwa kutoa mfano kwa Ronaldo baada ya kumpiga Crespo wakati wa mpira wa kona, kisha akampiga teke Edimar.
    Ronaldo appears to claim there is nothing wrong as the Brazilian defender goes down clutching his face
    Ronaldo akilalamika kana kwamba hajamfanya kitu beki huyo Mbrazil aliyeanguka chini
    In a final act of petulance, Ronaldo takes a backhand swipe at Crespo before being shown the red card
    Ronaldo akimchapa konde Crespo kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO AFUNGIWA MECHI MBILI KWA 'UBONDIA' LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top