• HABARI MPYA

    Tuesday, January 27, 2015

    ILALA WAING’OA IRINGA KOMBE LA TAIFA WANAWAKE

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MALKIA wa Mjini, Ilala Queens wametinga Nusu Fainali ya Kombe la Taifa Wanawake, baada ya kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Iringa katika mchezo wa Robo Fainali uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Salome George Mwakipesile alitangulia kuifungia Iringa dakika ya 40 na ushei, bao ambao lilidumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza katika mechi hizo zinazochezwa kwa dakika 80.
    Lakini kipindi cha pili, Ilala inayofundishwa na Rachel Pallangyo ambaye pia ni Mwandishi wa Habari wa magazeti ya Serikali, Habari Leo na Daily News ilizinduka na kufanikiwa kushinda mechi.
    Khadija Ally wa Ilala akimtoka Happy Mwambungu wa Iringa katika Robo Fainali ya Kombe la Taifa la Wanawake leo
    Wachezaji wa Ilala wakifurahia uishindi wao baada ya mechi

    Rose Mpoma alianza kuwainua vitini mashabiki wa Ilala waliojitokeza Uwanja wa Azam Complex kwa bao la kusawazisha dakika ya 50, kabla ya Meckline Sylvester kufunga la ushindi dakika ya 63. 
    Kwa matokeo hayo, Ilala itakutana na mshindi kati wa Mjini wenzao, Temeke au Mbeya, ambazo zinamenyana hivi sasa katika Robo Fainali ya mwisho.
    Mapema jana, Kigoma iliitoa Mwanza kwa kuichapa mabao 2-1, huku Pwani wakiigaragaza Tanga 5-2 na timu hizo zitakutana katika Nusu Fainali Alhamisi. 
    Kikosi cha Ilala kilikuwa; Hamisa Chande, Saraphina Peter/Maria Bayo dk27, Rose Mpoma, Khadija Ally, Mayciana Prosper, Batuli Mohammed, Zainab Mlenda/Jaqcueline Albert dk45, Hamida Fadhil, Fatuma Issa/Salma Masoud dk41, Madeline Sylvester/Aisha Kidunda dk66 na Ramla Said/Mariam Said dk41. 
    Iringa; Edna Mdelwa, Happy Mwambungu, Neema Nduye, Lucy London, Judith Nyato/Adolphina Mhenzi dk41, Amina Kyando, Margareth Lowokelo, Salome Mwakipesile na Winfrida Maketa.   
    Mgeni rasmi, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (katikati) akiwasalimia wachezaji wa Ilala kabla ya mechi

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ILALA WAING’OA IRINGA KOMBE LA TAIFA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top