• HABARI MPYA

    Tuesday, January 27, 2015

    KAZI IPO PANAMA NA BOOM FC AIRWING LEO LIGI YA MKOA DAR

    Na Omary Katanga, DAR ES SALAAM
    MECHI ya kiporo katika michuano ya Ligi ya mkoa wa Dar es salaam kati ya klabu za Panama FC dhidi ya Boom FC, itapigwa leo kwenye Uwanja wa Airwing, Ukonga ukiwa ni mchezo ambao utatoa fursa kwa DRFA kutangaza timu 18 zilizofanikiwa kutinga katika hatua ya 18 bora ya michuano hiyo.
    Michuano hiyo ya ligi mkoa wa Dar es salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36,inaingia katika hatua ya mwisho katika hatua ya mwisho ambayo itatoa wawakilishi wa mkoa Dar es salaam katika ligi ya mabingwa wa mikoa ya TFF.
    Kivumbi cha hatua ya 18 bora, kitaanza kutimkaFebruari 4, mwaka huu.

    Wakati huo huo, Ligi ya soka la wanawake kwa mkoa wa Dar es salaam inataraji kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao kwa kushirikisha jumla ya timu 12, zitakazoumana kuwania ubingwa huo.
    Itakumbukwa kwamba DRFA iliamua kusogeza mbele mashindano hayo ambayo yalikuwa yaanze Januari 16, mwaka huu kutokana na upungufu wa wachezaji kwa timu husika  ambao wengi wao wanashiriki mashindano ya kuwania kombe la Taifa Wanawake,ambayo sasa imeingia katika hatua ya robo fainali.
    Timu zote 12 zitakazoshiriki ligi hiyo ya mkoa wa Dar es Salaam, zitawekwa hadharani hapo baadaye.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAZI IPO PANAMA NA BOOM FC AIRWING LEO LIGI YA MKOA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top