![]() |
| Ronaldo kulia na Messi kushoto, je nani atacheka Jumamosi? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona |
WAKATI mechi ya wapinzani wa jadi Hispania 'Clasico' Jumamosi
kati ya Real Madrid na Barcelona inatarajiwa kutoa picha ya nani atakuwa
bingwa, lakini pia itakuwa ni vita ya mabao kati wachezaji wenye ‘rekodi chafu’
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Vinara Real wanamzidi pointi nne bingwa mtetezi, Barca zikiwa
zimebaki mechi tano La Liga kufikia ukingoni kuelekea mechi mechi hiyo Uwanja
wa Nou Camp na Ronaldo na Messi tayari wamefunga mabao 41 kila mmoja yaliyovunja
rekodi La Liga msimu huu.Mreno Ronaldo, ambaye awali aliweka rekodi ya mabao 40 msimu uliopita, amefunga mabao 53 katika mashindano yote, wakati Muargentina Messi, mtu aliyempokonya tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia na kukaa nahyo kwa miaka mitatu, amefunga mabao 63 kwenye mashindano yote, yakiwemo 14 kwenye Ligi ya Mabingwa.
Anakaribia kuvunja rekodi ya daima ya mabao katika Ligi kubwa Ulaya, mabao 67 yaliyofungwa na mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich, Gerd Mueller msimu wa 1972-73.
Pamoja na mechi hii ya ligi baina ya klabu hizo mbili tajiri duniani kuna uwezekano pia Real na Barca zikakutana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi ujao, Real ikiwania taji la 10 Ulaya na mabingwa watetezi, Barca wakiwania taji la tatu ndani ya miaka minne na la tano kwa ujumla.
Timu zote mbili zilifungwa katika mechi za kwanza za Nusu Fainali ugenini, Real ikilala 2-1 mbele ya Bayern Munich na Barca ikichapwa 1-0 na Chelsea London.
Mabingwa wa Hispania miaka mitatu iliyopita, Barca tayari wameifunga Real katika mechi zote mbili za Super Cup ya Hispania na Kombe la Mfalme msimu huu na pia walitoka nyuma na kushinda 3-1 kwenye mechi ya kwanza ya La Liga Desemba, mwaka jana.
Kama watamaliza ligi wakiwa wanalingana kwa pointi, bingwa ataamuliwa kulingana na matokeo ya mechi baina yao katika ligi hiyo na si wastani wa mabao.
Mechi zao zimekuwa hazikimaliki bila utata kama tuhuma kwa marefa kupendelea, kadi nyekundu na kadhalika. Jose Mourinho alimvaa na kocha Msaidizi wa Barca, Tito Vilanova na kutaka kumdhuru jichoni katika mechi ya kwanza msimu huu.
Akiwa katika msimu mzuri, kocha huyo Mreno anatarajiwa kumaliza utawala wa Barca, ingawa bado hajafikia mafanikio yaliyomjengea heshima alipokuwa akifanya kazi kwao Ureno, England na Italia.
HISTORIA YA UPINZANI:
Ronaldo dhidi ya Messi ni sehemu ya utamu wa mechi hiyo
kutokana na upinzani wao.Barca wanachukuliwa kama wawakilishi wazuri wa Catalonia, wakiwa maadui wa serikali ya ya Madrid, iliyo upande wa Real.
Vita huyo pia inafika hadi kwenye vyombo vya habari vya michezo Hispania, gazeti la Jijini Madrid na Marca na El Mundo Deportivo la Barcelona.
Mourinho aliwahi kuwa Kocha Msaidizi wa Real miaka ya 1990 wakati kocha wa sasa wa Barca, Pep Guardiola anachezea Barcelona.
Mourinho, amekuwa akirudia kusema Barca inabebwa na marefa na a meweza kumfunga Guardiola mara moja katika mechi 10 tangu ajiunge na Real akitokea Inter Milan mwaka 2010, ushindi wa 1-0 katika mechi iliyodumu kwa dakika 120, fainali ya Kombe la Mfalme mwaka jana.
Barca iliitoa Real katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, wakati pia waliitandika 5-0 katika La Liga katika mechi ya kwanza Mourinho kuiongoza Real Uwanja wa Nou Camp Novemba mwaka 2010.
"Yeye (Guardiola) ni mtu mwenye akili sana na anajua alifanyeje kushinda mechi nyingi kiasi hicho," alisema Mourinho kama bongostaz.blogspot.com inavyomnkuu katika Mkutano na Waandishi wa Habari baada ya mechi na Bayern.
"Anafahamu sawia vizuri jinsi gani alifanya," alisema Mreno huyo, ambaye alipigwa faini na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) msimu uliopita kwa kuituhumu bodi hiyo ya soka Ulaya kuipendelea Barca.
UBABE WA JUMLA...
Timu yoyote itakayoshinda Jumamosi itatimiza mechi 87 za 'Clasico'
kushinda katika mechi 219 walizokutana tangu walipokutana mara ya kwanza katika
Kombe la Hispania Mei 1902, dhidi ya 86 za mpinzani wake na sare 46.Real wamebakiza bao moja tu kuvunja rekodi yao wenyewe ya mabao katika La Liga ya mabao 107 iliyowekwa chini ya kocha raia wa Wales, John Toshack msimu wa 1989-90.
Nafasi mbili za juu katika Ligi ya Hispania, inaacha mwanya mkubwa na nafasi ya tatu kuendele kwa mara nyingine msimu huu, ambayo hakuna klabu nyingine imeweza kuifikia kwa muda mrefu.
Valencia iliyo katika Nusu Fainali ya Europa League inazidiwa pointi 29 na Barca katika nafasi ya tatu kuelekea mechi yao na Real Betis Jumapili na Malaga, inayocheza na Osasuna Jumatatu, inzidiwa pointi moja katika nafasi ya nne na Valencia



.png)
0 comments:
Post a Comment