• HABARI MPYA

    Sunday, April 29, 2012

    KILA LA HERI SIMBA SC LEO


    Simba kazi moja leo
    Imeandikwa na Clecence Kunambi; Tarehe: 28th April 2012 @ 14:59 Imesomwa na watu: 141; Jumla ya maoni: 0

        
    Image
    Kikosi cha Simba
    Habari Zaidi:
  • Simba kazi moja leo
  • Viongozi washtukia janja ya wazee Yanga
  • Timu ya Taifa gofu visingizio kibao
  • RC achukizwa Polisi kushuka daraja
  • Copa Coca-Cola yaanza Dodoma
  • Dereva Yanga azuiwa Arusha
  • TBL kudhamini ligi Zanzibar
  • Tanzania yatokota gofu Malawi
  • Watanzania wawili waombewa ITC wacheze Ulaya
  • Jeshi Stars, Magereza mabingwa wavu
  • Muhani awapa somo Simba kuiua Shandy
  • African Lyon pumzi muhimu leo
  • Wasanii, Twiga Stars kuvaana Dar es Salaam
  • Mwamuzi wa Azam, Mtibwa aondolewa
  • Wasudan watua, Sumaye kuibariki Simba Jumapili
  • Yanga yatambia kipigo cha Oljoro
  • Mechi ya Twiga Stars, Zimbabwe yafutwa
  • Uchaguzi RT wapigwa kalenda tena
  • Exim Bank yaichapa Diamond Trust
  • Bondia Salma aapa kummaliza Asha

  • Habari zinazosomwa zaidi:
  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
  • Balaa lingine kwa Chenge
  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
  • Vatican yamvua jimbo Askofu
  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
  • SIMBA leo inashuka kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza na timu ya Al Ahly Shandy ya Sudan kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka la Afrika(CAF).

    Wawakilishi hao wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa waliingia kwenye hatua hiyo baada ya kuiondoa kwenye mashindano hayo timu ya Entente Setif ya Algeria ugenini kwa faida ya bao la ugenini baada ya timu hiyo ya Algeria kushinda nyumbani kwa mabao 3-1.

    Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

    Kabla ya kukutana na Setif, Simba iliiondoa kwenye mashindano hayo timu ya Kiyovu ya Rwanda kwa mabao 3-2, hiyo ni kutokana na kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo uliochezwa Kigali, Rwanda na zilipokuja kurudiana Dar es Salaam Simba ilishinda kwa mabao 2-1.

    Al Ahly SDhandy mpaka kufikia hatua hiyo iliitoa timu ya Ferroviario ya Msumbiji na sasa inakabiliana na vinara hao wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara ugenini.

    Mshindi baina ya timu hizo kwenye mechi ya leo atajiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua inayofuata kwani timu hizo zitarudiana baada ya wiki mbili Khartoum Sudan.

    Ni mechi inayokutanisha timu mbili zenye mazingira tofauti kwenye mashindano hayo kwani Simba ina uzoefu na historia nzuri na mashindano hayo kwani mbali na kushiriki mara kadhaa, lakini pia iliwahi kufika hatua ya fainali na kulikosa kombe nyumbani kwa kufungwa mbao 2-0 na Stella Abdijan ya Ivory Coast mwaka 1993.

    Al Ahly Shandy ni timu ndogo isiyo na historia yoyote kwenye mashindano hayo kwani hii ni mara ya kwanza kushiriki.

    Mara nyingi Sudan imekuwa ikiwakilishwa na timu za El Hilal na El Merreikh kwenye mashindano makubwa ya Afrika.

    Kutokana na mazingira hayo, mchezo wa leo unagusa hisia tofauti tofauti miongoni mwa wadadisi wa mambo ya soka la Tanzania, kwani wapo watakaokuwa wanaamini Simba itakuwa na kazi rahisi dhidi ya Wanubi hao, lakini wapo pia watakaokuwa wanaamini mchezo wa leo
    hautabiriki na lolote linaweza kutokea.

    Lakini uhalisia wa mchezo wa soka ni kwamba hata siku moja haitabiriki pamoja na juhudi za wachambuzi wa mchezo huo kujaribu kutabiri matokeo yake mara kwa mara.

    Hivyo mechi hiyo ni ngumu na mwamuzi bado ataendelea kuwa dakika 90 za mchezo huo.

    Simba wanatakiwa kuupa uzito mkubwa mchezo wa leo ikibidi kupata mabao mengi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri pindi timu hizo zitakaporudiana wiki mbili zijazo nchini Sudan.
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KILA LA HERI SIMBA SC LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top