![]() |
| Oliech |
BODI ya sheria ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA)
imesema kwamba nyota wa Kenya, Dennis Oliech anastahili kuchukuliwa hatua za
kinidhamu kwa uamuzi wa kujitoa timu ya taifa.
Oliech, anayechezea timu ya Ligi Kuu Ufaransa, Ligue 1, AJ
Auxerre na ni Nahodha wa timu yake ya taifa, Harambee Stars, amejitoa timu ya
taifa wakati ikiwa katika maandalizi ya mechi ya kuwania tiketi ya kucheza
Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Togo Juni 16.Oliech anadai kiwango cha fedha ambacho hajabainisha kiwango kwa sababu picha yake ilitumika na wadhamini wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) katika tangazo la biashara.
Wadhamini, Kampuni ya Bia Afrika Mashariki na FKF wamesema mchezaji huyo hastahili kulipwa chochote kwa kuwa mkataba wa udhamini hausemi hivyo.
"Mkataba unamruhusu mdhamini kutumia picha za timu ya taifa katika promosheni za biashara zao. Lakini kwa sasa tunashughulikia mpango baina ya wachezaji na wadhamini," alisema Mwenyekiti wa FKF, Sam Nyamweya.
Mkurugenzi wa Sheria wa FIFA, Marco Villiger, amesema katika taarifa yake kwa FKF iliyoifikia bongostaz.blogspot.com kwamba mchezaji anatakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kama amekaidi wito wa timu ya taifa.
"Kwa sheria mama, kila mchezaji aliyesajiliwa na klabu anatakiwa kutikia wito wa chama cha soka kuiwaikilisha nchi yake," alisema jana Villiger.
Mchezaji mwingine mkubwa wa Kenya, MacDonald Mariga, anayechezea Parma ya Italia, ametofautiana na Shirikisho juu ya madai ya fedha zakezaidi ya shilingi Milioni 1 za Kenya alizokuwa akitumia kwa tiketi za kuja kujiunga na timu ya taifa.



.png)
0 comments:
Post a Comment