• HABARI MPYA

    Monday, April 30, 2012

    SAMATTA AIFUNGIA TENA MAZEMBE AFRIKA


    Samatta anafunga hapo mpira ushatimkia nyavuni, lango halionekani.

    MBWANA Ally Samatta, maarufu kama Sama Goal, jana aliibuka shujaa kwenye Uwanja wa Kibassa Maliba, baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa 2-0 kwa timu yake kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Tout Puissant Mazembe imeanza vizuri hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kushinda 2-0 dhidi ya El Merreikh ya Sudan mjini Lubumbashi.
    Wageni wanaonolewa na RICARDO waliuanza mchezo huo vizuri na mapema tu shuti lao kali la mpira wa adhabu liliokolewa na kipa KIDIABA na shambulizi la kwanza dakika ya 39 lilipaa juu ya lango.
    Kama ilivyokuwa dhidi ya Power Dynamos, safu ya ushambuliaji ya Mazembe inayoundwa na wakali kama MPUTU, Singuluma, Kalaba na SAMATA ilikuwa mwiba mkali.
    Mazembe ilipata kona sita wakati wapinzani wao hawakupata hata moja na katika kona hizo ni moja tu iliyozaa  matunda kwa SAMA GOAL kufunga dakika ya 22 kwa kichwa akiunganisha kona iliyochongwa na MPUTU.
    Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika Mazembe inayofundishwa na Lamine Ndiaye ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa bao hilo moja tu.
    Nahodha Tressor Mputu aliifungia Mazembe bao la pili dakika ya 70, akipiga shuti zuri nje ya eneo la penalti na mpira kutinga nyavuni upande wa kulia wa lango.
    Hakuna kilichobadilika katika dakika 20 za mwisho, licha ya nafasi kadhaa zilizoshindikana kutumiwa vema.
    Mazembe sasa inatakiwa kwenda kupigana kiume ugenini kulinda ushindi wake huu, kwani ni mwembamba.
    Samatta, Mtanzania aliyetokea Simba SC kujiunga na Mazembe katikati ya msimu uliopita, sasa ana mabao mawili katika Ligi ya Mabingwa ndani ya mechi mbili.
    Awali alifunga katika sare ya 1-1 na Power Dymanos ya Zambia, mchezo wa kwanza hatua ya 32 Bora, lakini sikku hiyo aliumia bega na akakosa mechi ya marudiano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA AIFUNGIA TENA MAZEMBE AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top