• HABARI MPYA

    Thursday, April 19, 2012

    MOROSINI AZIKWA, SOKA LAREJEA TALIA KAMA KAWA

    Di Natale
    MSHAMBULIAJI wa Udinese, Antonio Di Natale ameumizwa zaidi na kifo cha Piermario Morosini wiki iliyopita, lakini atarejea uwanjani wakati timu yake ikisafiri kwenda kucheza na Chievo Jumamosi, akitumaini kujitengenezea mazingira ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Italia Italia, alikuwa karibu mno na na mchezaji mwenzake huyo wa zamani, ambaye alipata matatizo ya moyo na kufariki dunia akiichezea Livorno katika mechi ya Serie B huko Pescara mwishoni mwa wiki iliyopita na ameanzisha mfumo maalum "Udinese per la vita", wa kumsaidia dada wa Morosini.
    Mazishi ya Morosini yalifanyika nyumbani kwake Bergamo Alhamisi na wakati mwili wake ukiwasili kanisani Jumanne jioni, mamia ya mashabiki wa klabu ya Atalanta walitoa heshima zao kwa mabango na bendera.
    "Mario alikuwa kama kaka kwangu," alisema Di Natale Jumatatu. "Alikuwa mtu babu kubwa ambaye alihangaika sana, na alimsaidia maisha dada yake (Maria Clara)."
    Mechi zote za Serie A ziliahirishwa mwishoni mwa wiki kwa heshima ya Morosini na wakati michuano inarejea, Di Natale amesema msimu huu ni mgumu sana na alipanga kustaafu msimu uliopita kutokana na kukosa muda wa kupumzika baada ya mechi.
    "Tunahitaji kuepuka kucheza mechi za karibu karibu... nimekuwa nikisema hivi kwa muda mrefu, ni nimezungumza juu ya hili na madaktari wa klabu yetu,"alisema.
    "Naendelea kusema hivi kwa madaktari na makocha.. afya zetu lazima zilindwe."
    Wakati Udinese inayoshika nafasi ya nne itasafiri kwenda Verona kumenyana na Chievo, Lazio inayoshika nafasi ya tatu itamenyana na Lecce ‘walio vizuri’ kwenye Uwanja wa Olimpico Jumapili.
    Timu zote hivi karibuni zimehusishwa na kashfa ya kupanga matokeo na wiki iliyopita beki wa Cremonese, Carlo Gervasoni alisema euro 400 000 zilitumika msimu uliopita baina ya klabu hizo huko Puglia, akimtaja Stefano Mauri kama kinara wa mchezo huo mchafu.
    Mechi kubwa mwishoni mwa wiki hii itafanyika Torino Jumapili Roma inayoshika nafasi ya tano ikimenyana na wenyeji Juventus, wakitumai kuwafungisha breki wapinzani wao hao wa muda mrefu na kupunguza idadi ya pointi wanazozidiwa na wapinzani wa jiji la Roma, Lazio.
    Juventus inaongoza ligi ikiizidi AC Milan pointi moja kileleni mwa Serie A, lakini timu ya Massimiliano Allegri inapewa nafasi kubwa ya kuifunga Bologna kwenye Uwanja wa San Siro mapema siku hiyo na Juve wanawezwa kuachwa kwa pointi mbili.
    Wanaoitia presha Roma ni Inter Milan na Napoli, ambaon wote wana pointi 48, wakati Inter watasafiri kwenda kumenyana na Fiorentina iliyo kwenye hatari ya kushuka daraja na Napoli itakuwa mwenyeji wa Novara.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOROSINI AZIKWA, SOKA LAREJEA TALIA KAMA KAWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top