• HABARI MPYA

  Tuesday, May 05, 2009

  MISS MZIZIMA KAMBI TAHAMIA SINZA


  WAREMBO wanaoshiriki shindano la Dar es Salaam (Mzizima) wamehamishia kambi yao ya mazoezi kwenye ukumbi wa hoteli ya Deluxe, Sinza mjini Dar es Salaam badala ya Break Point Outdoor katikatin ya jiji.
  Mratibu wa shindano hilo, Dina Ismail alisema mjini Dar es Salaam jana kwamba, sababu za kuhamishia kambi hiyo kutoka katikati ya jiji zimezingatia tatizo la foleni kutoka na kwenda na katikati ya Jiji.
  “Unajua Sinza kidogo ni eneo ambalo linafikika kwa urahisi, kwa hivyo tumeona tuwapunguzie mzigo warembo wetu kwa kuhamishia mazoezi hapa,”alisema.
  Hata hivyo, Dina alisema kama kawaida, wiki ya mwisho warembo hao watahamishia kambi yao kwenye ukumbi wa Afri- Centre, Ilala ambako ndiko shindano hilo litafanyika, Juni 6, mwaka huu.
  Dina alisema kwa ujumla maandalizi yanaendelea vizuri na wanatarajia shindano la Miss Dar es Salaam (Mzizima) mwaka huu litavunja rekodi ya mashindano ya vitongoji kama ilvyo kawaida yao.
  Uzinduzi wa Miss Dar es Salaam (Mzizima) ulifanyika Jumatatu katika mgawa wa Hadees Fast Food, jijini na kuhudhuriwa na wawakiklishi wa wadhamini wakuu wa shindano hilo, Emillian Rwejuna wa Vodacom na Kabula Nshimo wa Redd’s Original.Wadhamini wengine wa shindano hilo ni New Habari Media Group, Free Media Limited, Clouds FM Radio, Break Point Limited, Vuvuzela Company Limited, Hartman Productions
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MISS MZIZIMA KAMBI TAHAMIA SINZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top