• HABARI MPYA

  Thursday, May 21, 2009

  MISS MZIZIMA 2009 MAMBO BAMBAM
  BENDI ya Vibration Sound chini ya kinara wa gitaa la solo nchini kwa sasa, Elystone Angai, inategemea kuupamba usiku wa kumsaka kimwana wa Mzizima utakaofanyika katika ukumbi wa Africenter, Ilala jijini Dar es Salaa Juni 6 mwaka huu.
  Haya yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa Royal Modern Entertainment, Dina Zubeiry wakati alipoongea na Bingwa jijini Dar es Salaam.
  “Kila kitu kinaenda sawa na imeshathibishwa kwamba bendi hiyo itapanda jukwani siku hiyo kutumbuiza wapenzi wa burudani watakaokuja kushuhudia kusakwa kwa mrembo mpya wa Mzizima,” alisema Dina.
  Mbali na Vibration Sound ambayo inatamba na albumu ya ‘Homework’, siku hiyo kutakuwa na burudani nyingine za kukata na shoka kutoka kwa wasanii mbalimbali.
  Baadhi ya wasanii watakaoukuwapo siku hiyo ni Buibui, Barnabas na Pipi wote kutoka kikundi cha sanaa cha Nyumba ya Vipaja (THT).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MISS MZIZIMA 2009 MAMBO BAMBAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top