• HABARI MPYA

  Tuesday, May 05, 2009

  MAXIMO AVUNJA FUNGATE YA NGASSA


  KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Marcio Maximo, alimtenganisha winga wa Yanga, Mrisho Ngassa na mkewe, Latifa Abdul, takriban saa 48 tu tangu afunge naye ndoa, wakiwa kwenye fungate kwa kumtaka aingie kambini kujiandaa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Ngassa, aliyeoa Ijumaa mchana, alirejea kambini Taifa Stars siku ya Jumapili jioni na kumuachia upweke mkewe, Latifa.
  “Imenibidi kwenda kambini, kocha ameniita, fungate inaishia hapa,” alisema Ngassa Jumapili, alipozungumza na bongostaz kwa simu kutoka sehemu aliyokuwa amejichimbia na ‘asali wake wa moyo’.
  Stars ipo kwenye matayarisho ya mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambao ni mabingwa wa kwanza Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) iliyofanyika mwaka huu nchini Ivory Coast.
  Mchezo huo, unatarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ngassa alikuwa nchini Uingereza kufanya majaribio kwenye klabu ya West Ham United, ambako pamoja na kumridhisha kwa uwezo kocha wa timu hiyo, Gianfranco Zola, lakini amerudishwa nyumbani kuongeza mwili.
  Winga huyo wa Yanga, pia anatakiwa na klabu nyingine kadhaa za Ulaya, ikiwemo Charlton Athletic ya Uingereza pia, Marseille ya Ufaransa na Lov Ham ya Norway.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAXIMO AVUNJA FUNGATE YA NGASSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top