• HABARI MPYA

  Thursday, July 05, 2018

  WERASSON AWASILI DAR KUTUMBUIZA, CHRISTIAN BELLA AWAKATAZA WANAWE KUWA MWANAMUZIKI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
  MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Werrason Ngiama Makanda,  amewasili nchini kwa ajili ya kufanya maonyesho tofauti katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Dar es Salaam.
  Werrason aliyewasili majira ya saa sita mchana akipokelewa na mamia ya watu pamoja na msanii wa muziki wa dansi nchini King Dodoo na mratibu wa ziara hiyo Lengos VIP.
  Akizungumza baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA), Werrason amesema kuwa amekuja kukata kiu ya wapenzi wa muziki wa dansi nchini ambao walimkosa katika shoo iliyopita 
  Amesema kuwa shoo yake ya mwisho alishindwa kuja ila kwa sasa amekuja kuleta burudani iliyokosekana  baada ya kushindwa kufika.
  "Nimekuja kukata burudani ya wapenzi wa soka baada ya kukosekana kwa shoo ya mwisho ila sasa hivi nipo na nimeshafika hapa wajiandae kwa burudani,"amesema Werrason.

  Werrason Ngiama Makanda amewasili nchini kwa ajili ya kufanya maonyesho tofauti katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Dar es Salaam 

  Naye Mratibu wa ziara ya mwanamuziki huyo, King Dodoo Labuche alisema kuwa mwanamuziki huyo amewasili tayari na  ataondoka kesho mapema kuelekea Mkoani Arusha kwa ajili ya shoo ya Kwanza na kisha siku ya Jumamosi atakuwa mkoani Mwanza na ya mwisho atamalizia hapa Dar es Salaam.
  "Werrason atafanya Shoo ya kwanza mkoani Arusha siku ya Ijumaa ya Julai 6 na siku ya pili ya Julai 7, atakuwa mkoani Mwanza huku onyesho la mwisho litafanyika Mkoani Dar es Salaam'"amesema King Dodoo Labuche
  Alisema mkoani Arusha Mwamuziki huyo atafanya onyesho kwenye ukumbi wa Mjengoni Club, wakati Mwanza atafanya mambo yake kwenye ukumbi wa Rock City na Mkoa wa Dar es Salaam Life Park uliopo Mwenge (zamani Word Cinema).
  Werrason aliyeanzia katika bendi ya Wenge BCBG,  miongoni mwa wanamuziki wa Congo wanaopata nafasi za kupata mwaliko wa kuja kutoa burudani hapa nchini,  huku mratibu wa maonyesho hayo akiwataka mashabiki wajitokeze kupata burudani nzuri kutoka kwa nguli huyo.
  Wakati huo huo: Mwanamuziki mwingine Mkongo anayefanya shughuli zake nchini Tanzania, Christian Bella amesema hapendi kuona mtoto wake akifuata nyayo zake huku akihitaji apate elimu na kuja kuwa Daktari au waendesha Ndege.

  Christian Bella amerejea kutoka Marekani alipokwenda kutumbuiza katika Usiku wa Utamaduni wa Mswahili

  Bella alikwenda nchini marekani kwa ajili ya kufanya show amerejea jini  leo mchana.
  Mwanamuziki huyu alisema anapambana kuhakikisha vijana wake hao wawili Chris na Hans wanapata elimu na hapo baadae kuja mtu mkubwa nchini.
  "Mzazi wao sijapata elimu ya kutosha kutoka na mazingira magumu, lakini muda miaka ya sasa watoto wetu tunauwezo wa kuwasomesha hivyo wakazanie katika misingi ya elimu," alisema.
  Bella alisema ugumu wa muziki wa Afrika ndio sababu pekee ya kutotaka watoto wake kutokuwa wanamuziki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WERASSON AWASILI DAR KUTUMBUIZA, CHRISTIAN BELLA AWAKATAZA WANAWE KUWA MWANAMUZIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top