![]() |
| Van Persie |
NAHODHA wa Arsenal, Robin van Persie ametetea uamuzi wake
kutembelea hoteli waliyofikia timu ya Barcelona Jumatano, akiwahakikishia
mashabiki wa Gunners kwamba alikwenda kumtembelea mchezaji mwenzake wa
Uholanzi, Ibrahim Afellay.
Tetesi zilivuja kwenye vyombo vya habari kwamba mpachika
mabao huyo mwenye umri wa miaka 27 anataka kuhamia Camp Nou.
Mholanzi huyo alipigwa picha katika kambi ya Barcelona,
lakini amesema hakwenda huko kwa nia mbaya.
Van Persie alisema katika taarifa iliyoifikia bongostaz.blogspot.com
kwamba: “Ufafanuzi ni rahisi sana kwa kweli. Rafiki yangu mzuri sana Ibrahim
Afellay anachezea Barcelona."
“Baada ya msimu mbaya kwake akiwa majeruhi kwa muda mrefu,
hatimaye alirejea kwenye timu – na alipokuwa nje nilikuwa nawasiliana naye sana
tu, lakini sikumuona. Hii ilikuwa nafasi yangu kwenda kumtembelea rafiki yangu
wa karibu, kumuonyesha sapoti na kushikamana.
“Kwa bahati mbaya hii ikabidi iwe hotelini, kwa sababu
hakupewa ruhusa kuondoka. Nilikuwa nimevaa traksuti yangu ya Arsenal na tulikaa
chini mapokezi kuzungumza na kupata chakula – yeyote angeweza kutuona na
hakukuwa na kificho. Nashindwa kupata picha kila mmoja analihusisha hili na
kuhama!”
Van Persie pia aliwaweka wazi mashabiki kwamba fikra zake juu ya
mustakabali wake hazijabadilika katika wiki za karibuni na atatoa msimamo wake
mwishoni mwa msimu.
“Kuetembelea hotelini lilikuwa suala moja la kijamaa na
halikuwa na chochote juu ya mustakabali wangu wa kazi,” alisema Nahodha hyuyo.
“Nina maisha ya kijamaa pembeni ya soka, pia hata kama mke
wangu akiniambia hivyo, wakati fulani haionekani kama hivyo! Hakuna kilichobadilika
akilini, kwamba nia yangu ni kujadili mustakabali wangu mwishoni mwa msimu,”alisema.



.png)
0 comments:
Post a Comment