| Wachezaji wa Ngorongoro wakishangilia |
TIMU ya taifa ya soka ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa
miaka 20, Ngorongoro Heroes imejiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele katika
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika, baada ya kuibwaga kwa
mabao 3-1 Sudan jioni hii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shukrani kwao, Thomas Ulimwengu, Ramadhani Singano ‘Messi’ na
Simon Msuya walioifungia mabao hayo Ngorongoro inayofundishwa na kocha
Mdenmark, Kim Poulsen.
Kwa matokeo hayo sasa, Ngorongoro inahitaji hata sare au
kufungwa si zaidi ya 1-0 kwenye mchezo wa marudiano na Sudan, ambayo jioni hii
bao lake la kufutia machozi lilifungwa na Sharafeldin Shaiboub, ili kusonga
mbele.
Ngorongoro wana kazi ngumu bado, kwani bao la ugenini walilopata
leo- ina maana wakishinda 2-0 kwenye mchezo wa marudiano kwao, watasonga mbele.
Pouslen aliiambia bongostaz.blogspot.com kwamba
amefurahishwa na matokeo na anawapongeza vijana wake, lakini akakiri ana kazi
ngumu bado mbele.
Poulsen alisema wameiona Sudan inavyocheza na watafanyia kazi
mapungufu yao ili kuhakikisha wanaitoa timu hiyo na kusonga mbele.



.png)
0 comments:
Post a Comment