• HABARI MPYA

    Saturday, April 21, 2012

    REAL YAISHUGHULIKIA BARCA, NI KAMA TAYARI MABINGWA

    Pati la ushindi Real
    Ozile akipongezana na Ronaldo baada ya bao la ushindi

    Lionel Messi (kulia) chini ya ulinzi wa Pepe.
     Ronaldo wa Real akimtoka Sergio Busquets wa Barca kushoto
    Cristiano Ronaldo akimtoka Carles Puyol wa FC Barcelona.
    REAL Madrid wapo karibu mno na ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga wakihitaji kushinda mechi moja tu zaidi ili kujihakikishia taji hilo.
    Hiyo inafuatia ushindi wa mabao 2-1 leo kwenye Uwanja wa Camo Nou katika mchezo wa marudiano wa La Liga.
    Zikiwa zimebaki mechi nne ligi hiyo kuisha, Real sasa wanaizidi pointi saba Barca.
    Vijana wa Jose Mourinho walipania haswa leo na hawakuwa wenye kutaka mzaha hata kidogo, kwani iliwachukua dakika 17 tu kupata bao la kwanza, mfungaji S. Khedira.
    Barca walirudi kwenye vyumba vya kupumzikia mbele ya maelfu ya mashabiki wao wakiwa vichwa chini kutokana na kuwa nyuma kwa bao hilo.
    Kipindi cha pili Barca walilazimika kusubiri hadi dakika ya 70, kupata bao la kusawazisha, mfungaji Sanchez.
    Wakati wengi wakiamini historia ya Barca kutoka nyuma mbele ya Real na kushinda itaendelea, mwanasoka bora wa zamani wa dunia, Mreno Cristiano Ronaldo alibatilisha imani hiyo.
    Dakika tatu tu tangu Sanchez aifungie Barca, Ronaldo aliifungia Real bao la ushindi kufuatia kazi nzuri ya Ozil.
     MSIMAMO WA LA LIGA 2011-12
     TIMUGPWDLPtsGFGAGD 
     Real Madrid332742851072978
     Barcelona33256281962472
     Valencia33141095250428
     Málaga33156125149463
     Levante33146134847461
     Osasuna3311139463753-16
     Athletic Bilbao331112104548444
     Atlético Madrid33129124544413
     Sevilla33129124540382
     Espanyol Barcelona33129124543430
     Getafe3312912453844-6
     Mallorca34111013433641-5
     Real Betis3312615424045-5
     Rayo Vallecano3412418405060-10
     Real Sociedad3310914394049-9
     Villarreal3381213363447-13
     Granada3310617363049-19
     Zaragoza348719312960-31
     Sporting de Gijón348719313564-29
     Racing Santander3341415262452-28
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REAL YAISHUGHULIKIA BARCA, NI KAMA TAYARI MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top