![]() |
| Borussia Dortmund katika pati lao la ubingwa |
KLABU ya Borussia Dortmund usiku huu imetetea ubingwa wake
wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
wapinzani wao, Borussia Monchengladbach hiyo ikiwa ni mara ya pili mfululizo
kutwaa taji hilo.
Awali, ilionekana kama mbio za ubingwa zingeendelea kabla ya
Dortmund kushuka kwenye Uwanja wa Signal Iduna Park, kutokana na Bayern Munich
kushinda 2-1 dhidi ya Werder Bremen katika mchezo uliotangulia.
Lakini haikuwa hivyo kwa Dortmund baada ya Ivan Perisic na
Shinji Kagawa kuifungia mabao timu yao hiyo na kuihakikishia kutwaa mara mbili
mfululizo taji hilo, hiyo pia ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1997, na mara
ya tatu katika historia ya klabu hiyo.
Taji hilo pia ni la pili mfululizo kwa kocha Jurgen Klopp
katika Bundesliga na kuzidi kujijengea heshima miongoni mwa makocha vijana
nchini humo.
BVB sasa imebakiza mechi mbili kukamilisha msimu wa
Bundesliga, dhidi ya Kaiserslautern na Freiburg.
Baadaye itamenyana na Bayern katika fainali ya michuano ya DFB
Pokal, ambayo kama wakishinda itakuwa ni mara ya kwanza kwao kutwaa ubingwa wa
Kombe hilo sambamba wa Ligi Kuu.



.png)
0 comments:
Post a Comment