![]() |
| MAREHEMU KANUMBA |
BAADA ya kifo cha nyota wa filamu za Swahiliwood, Steven
Kanumba, biashara nyingi zimeibuka zikitumia picha na jina la Kanumba huku
familia yake ikishuhudia biashara hizo zikifanyika bila kufaidika na chochote.
Biashara zilizotawala awali ilikuwa ni fulana, kofia,
vitabu, leso na picha zake. Kutokana na hali hiyo, familia yake kupitia Shirikisho
la Wasanii (TAFF) ilitangaza biashara hizo kusitishwa mara moja na wale
watakaohitaji kutengeneza bidhaa yoyote inayomhusu Kanumba kuwasiliana familia
yake kwanza.
Pamoja na agizo hilo watengenezaji wa vitabu wamekaidi.
Wiki hii TAFF kutumia kikosi maalum kinachofanya msako na
kukamata kazi bandia, imeanza zoezi la kukamata kazi hizo pamoja na vitabu
hivyo baada ya kupewa agizo na mama mzazi wa marehemu, Florence Mtegoze, kuwa
hawaruhusu chochote kufanyika bila idhini ya familia.
Kikosi kazi kilifanikiwa kuwakata baadhi ya wauzaji wa
vitabu katika maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam na kufikishwa kituo cha
polisi.
Shirikisho limeanza kazi kulinda haki za wasanii wake kama
unavyoona tayari tumefungua kesi kuhusu kazi za marehemu Kanumba zilizochapishwa
bila idhini ya familia yake, alisema Rais wa shirikisho hilo, Simon
Mwakifwamba.
Lakini hatuishii hapo tu kwani tayari tuna mkakati wa kuanza
pia kukamata kazi bandia za filamu hasa kwa wale ambao watakuwa wakitoa
ushirikiano kwa shirikisho ikiwa ni taarifa na kuonyesha hujuma hizo kutoka
upande wowote, filamu, vitabu.
GAZETI LA MWANASPOTI



.png)
0 comments:
Post a Comment