• HABARI MPYA

    Thursday, June 10, 2021

    HALMASHAURI YA GEITA KUJENGA UWANJA WA MICHEZO KWA GHARAMA YA SH. BILIONI 1.9 UTUMIKE KWENYE LIGI KUU

    Na Alphonce Kabilondo, GEITA
    HALMASHAURI ya Mji wa Geita Mkoani Geita imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 1.9 kwa ajili ya kujenga Uwanja mpya wa mpira utakaotumika katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambao utakuwa na uwezo wa kuingiza watu zaidi ya 18,000.
    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Mhandisi Felix Nlalio ametoa taarifa ya ujenzi wa uwanja huo mbele ya kamati ya siasa ya wilaya ya Geita ilipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.
    Kaimu Mkurugenzi huyo amesema kuwa mchakatao wa kumpata mkandarasi wa kujenga uwanja huo umeshamilika na kwamba halmashauri imetenga fedha hiyo ambayo ni mapato ya ndani pamoja na shilingi bilioni moja ambayo ni fedha ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii CSR kutoka Mgodi waa GGML.



    Alisema kuwa wakati ujenzi wa uzio ukiendelea utaenda sanjari na usanifu wa majukwaa na kupanda nyasi za (ukoka) na baadae zitawekwa nyasi za bandia ambapo ujenzi huo unatarajia kukamilika kwa kipindi cha miezi minne.
    Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilayani Geita, Barnabas Mapande alisema kuwa  mbali na wananchi kupata nafasi kushuhudia burudani ya soka kufuatia mitanange ya timu za Ligigi Kuu  itakayokuwa ikiendeea katika uwanja huo pindi utakapokamilika, halmashuri pia itakusanya mapato.
     ''Uwanja huu ni muhimu kwa wana Geita kwa kuwa sasa tunayo timu ya Geita Gold FC ambayo imefuzu kushiriki michezo ya Ligi Kuu, hivyo uwanja ukamilike haraka ''alisema mwenyekiti huyo .
    Aidha Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwalimu Fadhili  Juma alisema kuwa kiu kubwa ya wanageita ni kushudia ligi kuu inachezwa  kwenye dimba la Geita.
    Mkuu huyo alisema kuwa hivikaribuni Rais wa shirikisho la soka Nchini TFF Wallace Karia  alifika Geita na kutembelea eneo la Magogo kata ya Bombambili  unapojengwa uwanja huo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kuleta watalaamu waliobobea kusanifu viwanja vya soka.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HALMASHAURI YA GEITA KUJENGA UWANJA WA MICHEZO KWA GHARAMA YA SH. BILIONI 1.9 UTUMIKE KWENYE LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top