• HABARI MPYA

  Saturday, December 17, 2016

  NDANDA YAIMARISHA BEKI NA KIUNGO KUIVAA SIMBA

  Na Mwandishi Wetu, MTWARA
  TIMU ya Ndanda FC ya Mtwara imesajili wachezaji wawili tu wapya katika dirisha dogo kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Msemaji wa Ndanda FC, Idrisa Bandari aliiambia Bin Zubeiry Sports - Online jana kwamba wachezaji hao wawili wapya ni beki wa kati Ayoub Shaaban na kiungo Ismaill Mussa, ambao wote ni wachezaji huru.
  Bandari alisema wawili hao tayari wapo kambini na wenzao kwa maandalizi ya mwisho mwisho ya mchezo wao wa kwanza wa mzunguko wa pili dhidi ya Simba SC kesho Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
  Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Bandari alisema kwamba yanaendelea vizuri na wana matumaini makubwa ya kuwafunga Simba.
  Ndanda ilimaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ikiwa inashika nafasi ya 10 kwa pointi zake 19, wakati Simba ilimalizia kileleni kwa pointi zake 35, mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDANDA YAIMARISHA BEKI NA KIUNGO KUIVAA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top