• HABARI MPYA

  Wednesday, December 14, 2016

  MAAMBO YAANZA KUFUKUTA KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  CHAMA  cha Soka Zanzibar (ZFA) kimetaja Kamati ya kusimamia mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup) ambayo  imezinduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na MichezoOmar Hassan Omar ‘King’..
  Mashindano ya Mapinduzi Cup yatakayoshirikisha timu tisa kutoka Uganda, Tanzania Bara na wenyeji Zanzibar yatafanyika katika uwanja wa Amani kuanzia  tarehe 30 mwezi huu.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi ni Sharifa Khamis na Katibu wa Kamati hiyo ni Khamis Abdalla Said.
  Wajumbe wa Kamati ni Ali Khalil Mirza, Khamis Mzee Ali, Juma Mmanga, Ravia Idarous Faina, Mohammed Ali, Mohammed Ali Hilal, Issa Mlingoti Ali, Dk. Ally Saleh Mwinyikai na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Omar Hassan Omar ‘King’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAAMBO YAANZA KUFUKUTA KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top