NAHODHA wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Renatus Njohole amesikitishwa na kifo cha aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Sylvester Marsh.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo kutoka Onnens, Vaud, Uswisi anakoishi na kucheza soka, Njohole amesema kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Marsh.
“Taifa limempoteza mtu muhimu. Namjua mwalimu wa Marsh na nimekuwa nikifuatilia juhudi zake, kwa kweli alijitolea sana kwa maendeleo ya soka,”amesema Njohole.
Njohole mwenye umri wa miaka 34 sasa, aliwahi kufanya kazi kidogo na Marsh, katika timu ya taifa, Taifa Stars mwaka 2007 alipokuwa Msaidizi wa Mbrazil, Marcio Maximo.
Marsh alifariki dunia Alfajiri ya jana katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya saratani ya koo, ambayo yaliibuka mwaka jana.
Mwili wa marehemu utaagwa kesho kuanzia Saa 4:00 asubuhi Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa Mwanza kwa mazishi.
Kwa sasa, Njohole anachezea FC Bavois tangu mwaka 2010, baada ya awali kuchezea timu za Milambo ya Tabora mwaka 1997 hadi
1998 alipohamia Simba SC ambako alicheza hadi 1999 alipohamia Yverdon Sports ya Uswisi.
Mwaka 2004 alihamia FC Valmont alikocheza hadi 2005 alipohamia FC Baulmes ambako alicheza hadi 2007 akahamia FC Le Mont ambayo nayo aliichezea hadi 2010 akahamia klabu yake ya sasa, FC Bavois.

![]() |
| Renatus Njohole kushoto akiwa na rafiki zake Uwanja wa Camp Nou hivi karibuni kushuhudia mechi ya Barcelona nchini Hispania |
Njohole mwenye umri wa miaka 34 sasa, aliwahi kufanya kazi kidogo na Marsh, katika timu ya taifa, Taifa Stars mwaka 2007 alipokuwa Msaidizi wa Mbrazil, Marcio Maximo.
Marsh alifariki dunia Alfajiri ya jana katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya saratani ya koo, ambayo yaliibuka mwaka jana.
Mwili wa marehemu utaagwa kesho kuanzia Saa 4:00 asubuhi Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa Mwanza kwa mazishi.
Kwa sasa, Njohole anachezea FC Bavois tangu mwaka 2010, baada ya awali kuchezea timu za Milambo ya Tabora mwaka 1997 hadi
1998 alipohamia Simba SC ambako alicheza hadi 1999 alipohamia Yverdon Sports ya Uswisi.
Mwaka 2004 alihamia FC Valmont alikocheza hadi 2005 alipohamia FC Baulmes ambako alicheza hadi 2007 akahamia FC Le Mont ambayo nayo aliichezea hadi 2010 akahamia klabu yake ya sasa, FC Bavois.

.png)
0 comments:
Post a Comment