• HABARI MPYA

    Sunday, March 15, 2015

    NDONDI UWANJA WA NDANI WA TAIFA LEO, KARAMA NA MAUGO, KASEBA NA MBELWA, MASHALI NA PAZI

    Thomas Mashali wakati wa kupima uzito jana
    MABONDIA Karama Nyilawila na Mada Maugo wanapanda ulingoni kuzipiga katika pambano la raundi 10, uzito wa Super Middle Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hilo linakuwa pambano la marudiano kwa wawili hao, baada ya awali kukutana ulingoni Aprili 25, mwaka 2009 na Karama akamshinda Maugo kwa pointi ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa, Dar es Salaam.
    Siku hiyo, Jaji Boniface Wambura alitoa ushindi wa pointi 98-97 kwa Nyilawila, Kulwa Makaranga 99-96 na Michael Buchato akatoa 99-98. 
    Katika zoezi la kupima uzito jana, nusura wawili hao wazichape ‘kavu kavu’ wakati wa kutambiana. Mbali na pambano hilo, kutakuwa na mapambano kadhaa ya utangulizi yenye mvuto pia.
    Thomas Mashali atamkabili Abdallah Pazi pambano la uzito wa Middle, wakati Japhet Kaseba atapambana na Saidi Mbelwa uzito wa Super Middle pia.
    Japhet Kaseba kulia na Said Mbelwa kushoto wakitunishiana misuli jana wakati wa kupima uzito

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDONDI UWANJA WA NDANI WA TAIFA LEO, KARAMA NA MAUGO, KASEBA NA MBELWA, MASHALI NA PAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top