• HABARI MPYA

    Saturday, March 14, 2015

    MAN CITY ‘WAUWEKA REHANI’ UBINGWA ENGLAND, WAGONGWA NA VIBONDE 1-0

    MATUMAINI ya Manchester City kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya England yamezidi kufifia baada ya usiku huu kufungwa bao 1-0 na Burnely Uwanja wa Turf Moor.
    Kipigo hicho kinaifanya City ibaki na pointi zake 58 baada ya kucheza mechi 29, wakiizidi kwa pointi moja Arsenal iliyocheza mechi 29 pia.
    Chelsea wanaendelea kujinafasi kileleni kwa pointi zao 63 baada ya kucheza mechi 27, wakati Manchester United ni ya nne kwa pointi zake 53 za mechi 28.
    Bao pekee lililoizamisha City leo lilifungwa na 
    George Boyd dakika ya 61 na sasa kocha Manuel Pellegrini anazidi kukiweka ‘rehani’ kibarua chake Etihad.
    Kikosi cha Burnley kilikuwa; Heaton, Trippier, Duff, Shackell, Mee, Boyd, Arfield, Jones, Barnes, Vokes/Ward dk87 na Ings/Reid dk90.
    Man City; Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Jesus Navas, Toure/Lampard dk81, Fernandinho, Silva/Jovetic dk74, Dzeko/Bony dk63 na Aguero.
    City players can't hide their disappointment after another lacklustre display
    Wachezaji wa Manchester City wakiwa taabani baada ya kipigo cha Burnley

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2994997/Burnley-1-0-Manchester-City-George-Boyd-screamer-sinks-lacklustre-Blues-hands-title-advantage-Chelsea.html#ixzz3UOYFmwTc 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY ‘WAUWEKA REHANI’ UBINGWA ENGLAND, WAGONGWA NA VIBONDE 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top