ARSENAL imejiweka sawa nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya West Ham United jioni hii Uwanja wa Emirates, London.
Ushindi huo, unaifanya Arsenal ifikishe pointi 57 baada ya kucheza mechi 29, nyuma ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 58 za mechi 28 na vinara, Chelsea wenye pointi 63 za mechi 27. Man United sasa ya nne kwa pointi zake 53 za mechi 28.
Olivier Giroud alifunga bao lake la sita katika mechi saba akiifungia bao la kwanza The Gunners dakika ya 45, kabla ya Aaron Ramsey kufunga la pili dakika ya 81 na Mathieu Flamini la tatu dakika ya 84.
Katika mchezo huo, Refa Chris Foy alibadilishwa na msaidizi wake Anthony Taylor kipindi cha pili katikati.
Kikosi cha Arsenal kilkikuwa; Ospina, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Ramsey, Coquelin, Walcott/Cazorla, Ozil/Flamini, Sanchez/Welbeck na Giroud.
West Ham: Arian, O'Brien, Kouyate, Cresswell, Downing, Noble/Nene, Song, Nolan, Jarvis/Amalfitano na Sakho.
Olivier Giroud akienda hewani kushangilia baada ya kuifungia Arsenal katika ushindi wa 3-0 dhidi ya West Ham leo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2994864/Arsenal-3-0-West-Ham-Olivier-Giroud-Aaron-Ramsey-Mathieu-Flamini-target.html#ixzz3UNzCbx7f


.png)
0 comments:
Post a Comment