• HABARI MPYA

    Tuesday, November 25, 2014

    SOUTHAMPTON YA WANYAMA YAIPUMULIA CHELSEA KILELENI

    IKIONGOZWA na kiungo mahiri Mkenya, Victor Wanyama, Southampton imefanikiwa kuvuna pointi moja ugenini baada ya sare ya 1-1 na wenyeji Aston Villa usiku wa jana Uwanja wa Villa Park.
    Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya England, Gabriel Agbonlahor aliwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 29 akitumia vizuri makosa ya kipa Fraser Forster.
    Nathaniel Clyne aliisawazishia Southampton zikiwa zimebaki dakika tisa mchezo kumalizika na sare hiyo inafanya wageni hao wabaki wanazidiwa pointi sita na vinara wa Ligi Kuu, Chelsea, wakati Villa wanapandaa juu ya Hull nafasi ya 16.
    The England international (right) goes to celebrate his late equaliser in front of the travelling Southampton supporters at Villa Park

    Nathaniel Clyne kulia akishangilia baada ya kuifungia Southampton bao la kusawazisha jana Uwanja wa Villa Park

    Watu 25,311 tu walihudhuria mechi hiyo- hayo yakiwa mahudhurio mabovu zaidi tangu walipomenyana na Sheffield Wednesday Desemba 1999 walipocheza mbele ya watu 23,885.
    Kikosi cha Aston Villa kilikuwa; Guzan, Hutton, Okore, Clark, Cissokho, Westwood, Sanchez/Bent dk74, Weimann, N’Zogbia/Richardson dk64, Cleverley na Agbonlahor.
    Southampton; Forster, Clyne, Fonte, Alderwiereld, Bertrand, Wanyama, Schneiderlin, Tadic, Long/Cork dk89, Mane/Mayuka dk79 na Pelle.
    Villa midfielder Carlos Sanchez (centre) battles his way past Clyne (left) and Victor Wanyama during their Premier League encounter
    Kiungo wa Villa, Carlos Sanchez akipasua katikati ya Clyne (kushoto) na Victor Wanyama jana

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2847863/Aston-Villa-1-1-Southampton-Nathaniel-Clyne-s-late-equaliser-cancels-Gabriel-Agbonlahor-s-opener-visitors-draw.html#ixzz3K32nPeoh 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SOUTHAMPTON YA WANYAMA YAIPUMULIA CHELSEA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top