• HABARI MPYA

    Tuesday, November 18, 2014

    PIGO REAL MADRID, LUKA MODROIC NJE WIKI TANO BAADA YA KUUMIA JUZI AKILITUMIKIA TAIFA

    NYOTA wa Croatia, Luka Modric atashindwa kuichezea Real Madrid katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia baada ya kulazimika kutolewa nje juzi dakika ya 27 akiichezea yake ikitoa sare ya 1-1 na Italia.
    Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 aliumia nyonga wakati anakimbilia mpira na kurudishwa benchi, huku dalili zikionyesha hataweza kucheza mechi ijayo ya kufuzu Euro 2016 mjini Milan.
    Modric alipata huduma ya kwanza uwanjani, lakini haikumsaidia na akatolewa nafasi yake akiingia kinda anayeibuka vizuri, Mateo Kovacic anayechezea Inter Milan.
    Kituo cha Radio mjini Madrid, El Partido de las 12 kimeripoti kwamba, mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham anaweza kuwa nje kwa wiki tano, ambayo itamfanya asionekane uwanjani hadi Januari. 
    Kiungo wa Croatia, Luka Modric (mbele kulia) aliumia Jumapili akiichezea timu yake ya taifa dhidi ya Italia

    MECHI AMBAZO MODRIC ANAWEZA KUZIKOSA

    Novemba 22 - Eibar vs Real Madrid (La Liga)
    Novemba 26 - Basle vs Real Madrid (Ligi ya Mabingwa)
    Novemba 29 - Malaga vs Real Madrid (La Liga)
    Desemba 2 - Real Madrid vs Cornella (Kombe la Mfalme) 
    Desemba 6 - Real Madrid vs Celta Vigo 
    Desemba 9 - Real Madrid vs Ludogorets (Ligi ya Mabingwa) 
    Desemba 16 - Real Madrid vs Cruz Azul or Western Sydney Wanderers (Klabu Bingwa ya Dunia)
    Desemba 20 - Fainali Klabu Bingwa ya Dunia 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO REAL MADRID, LUKA MODROIC NJE WIKI TANO BAADA YA KUUMIA JUZI AKILITUMIKIA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top