![]() |
| Dk Mwinyihajji Makame akizungumza na BIN ZUBEIRY |
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Zanzibar, Dk Mwinyihajji Makame amesema kwamba Tanzania ina vipaji
sana vya soka, lakini kwa sasa kinachokosekana ni uongozi bora na ndiyo maana mchezo
unashuka.
Akizungumza na bongostaz.blogspot.com jana katika hoteli ya
Zanzibar Beach Resort visiwani Zanzibar, Dk Makame amesema kwamba vipaji vipo,
lakini lazima jitihada za kuwekekeza kwenye soka ya Vijana ziwe za dhati.
Alisema anapongeza sera za sasa za Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kwamba kila klabu lazima iwe na timu ya vijana ndipo, iruhusiwe
kucheza Ligi Kuu, lakini ameomba mpango huo utiliwe mkazo.
Hata hivyo, Dk Makame amesikitikshwa na desturi ya TFF
kuonekana kujali zaidi Simba na Yanga au Dar es Salaam pekee na kusahau mikoa
ikiwemo Zanzibar, hali ambayo imechangia kushuka kwa soka ya mikoani na kuathiri
maendeleo ya soka ya nchi hii kwa ujumla.
“Nchi hii ina vipaji sana, tangu zamani, mimi nakumbuka
miaka ya 1970 ilikuja hii timu ya West Brom Albion (ya England) ikacheza mechi
mbili za kirafiki, ilicheza na timu ya kombaini ya Dar es Salaam, ikacheza na
taifa kombaini, ambayo haikuhusisha wachezaji wa Dar es Salaam.
Ulichezwa mpira mkubwa sana na timu zote zilitoka sare na
WBA,” alisema.
Dk Makame amesema ukirejea Fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika mwaka 1980 nchini N igeria ambazo ni fainali pekee za michuano hiyo kwa
Tanzania kushiriki, wachezaji wa mikoani wengi walikuwamo kikosini.
“Kulikuwa kuna wachezaji wa Tanga, Morogoro, Tabora na Zanzibar
na kadhalika, haikuwa wachezaji wa Dar es Salaam pekee kama ilivyo sasa.
Thuwein Ally aliisaidia sana timu na ndiye aliyefunga mabao
yetu yote kule, huyu chimbuko lake na hapa (Zanzibar). Sasa lazima TFF iweke
mikakati ya kuisaidia mikoa kuzalisha vipaji na kuviendeleza na kuacha kuanglia
Dar es Salaam pekee,”alisema.



.png)
0 comments:
Post a Comment