RAY ATINGA POLISI KULALAMIKA KUPAKAZIWA KUMUUA KANUMBA, MLIMBWENDE ASWEKWA LUPANGO


Mange Kimambi
ALIYEKUWA mwandaaji wa shindano la urembo la Miss Dar Indian Ocean, Mange Kimambi amekatwa na Jeshi la Polisi Kinondoni kwa tuhuma za kumthumu mwigizaji maarufu nchini, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuhusika na mauaji ya mwigizaji mwenzake Steven Kanumba.
Akizungumza na bongostaz.blogspot. com, Kamanda wa Polisi Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Charles Kenyella, amesema Ray alishitaki kituo cha Polisi Oysterbay kuhusu Mange, kuandika tuhuma hizo kwenye blog yake, iitwayo U-turn.
 “Mange tulimshikilia hapa kwetu tangu jana (juzi), ila leo tumemwachia kwa dhamana na uchunguzi unaendelea,” alisema.
bongostaz.blogspot.com inaendelea kuwatafuta Mange na Ray kuzungumzia kesi yao.
Share on Google Plus

About Mahmoud Zubeiry

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
Post a Comment