![]() |
| Dioniz Malinzi |
MWENYEKITI wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz
Malinzi anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika kwa siku mbili
(Aprili 21 na 22 mwaka huu) kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es
Salaam.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace
Wambura ameiambia bongostaz.blogspot.com
Kwamba Wajumbe wa mkutano huo watawasili jijini kesho
(Aprili 20 mwaka huu) na watafikia kwenye hoteli ya Royal Valentino. Wajumbe
wanatoka katika vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu za
Ligi Kuu ya Vodacom.
Amesema Mkutano huo utakaoanza saa 3 asubuhi utakuwa na
ajenda kumi na moja. Baadhi ya ajenda hizo ni hotuba ya Rais wa TFF, taarifa ya
utendaji ya mwaka 2011, bajeti ya mwaka 2012 na taarifa ya ukaguzi wa hesabu
(audited accounts).
.jpg)


.png)
0 comments:
Post a Comment